Makari wa Collesano

Makari wa Collesano (Collesano, Sicilia, 915 hivi - Oliveto Citra, Campania, 16 Desemba 1000) alikuwa mmonaki, na hatimaye abati, wa Ukristo wa Mashariki[1] katika Italia ya leo[2].

Hata Kristofa na Kali, wazazi wake na Saba, kaka yake, walijiunga na monasteri ya Wabazili halafu wakasaidiana naye kueneza umonaki huo katika sehemu mbalimbali za Italia Kusini iliyozidi kuvurugwa na wavamizi Waislamu. Hatimaye alirudi kuishi kama mkaapweke.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, sawa na familia yake yote.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Desemba[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Lynn White Jr. "The Byzantinization of Sicily." The American Historical Review. Vol. 42, No. 1 (Oct., 1936). p. 5.
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/81740
  3. Martyrologium Romanum
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.

.