Margaret Clitherow

Margaret Clitherow (155625 Machi 1586) alikuwa mwanamke Mwingereza ambaye, kwa ruhusa ya mume wake, alibadilisha imani yake ya dini kutoka Ushirika wa Anglikana kuingia Kanisa Katoliki.

Margaret Clitherow, the Pearl of York.

Kwa vile aliwaficha mapadri nyumbani mwake na kuhudhuria misa ya Kikatoliki, alifungwa mara kadhaa katika dhuluma ya malkia Elizabeti I, akashtakiwa mahakamani lakini alikataa kujitetea ili asisababishe mahakimu wafanye dhambi ya kumpa adhabu ya kifo, hivyo akauawa kwa kubondwa mwili mzima na jiwe kubwa.

Mwaka 1970 alitangazwa na Papa Paulo VI kuwa mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake ni tarehe 25 Machi[1].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Peter Lake and Michael Questier: The Trials of Margaret Clitherow: Persecution, Martyrdom and the Politics of Sanctity in Elizabethan England: New York/London: Continuum: 2011|: ISBN 1-4411-0436-4

Viungo vya nje hariri

Margaret hariri

Watoto hariri

Mahali hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.