Massa Candida (walifariki 253-260) ni jina la kundi la Wakristo 300 hivi wa karne ya 3 waliofia dini yao huko Utica kwa kuwa walikataa kutoa sadaka ya ubani kwa miungu ya Roma kama walivyoagizwa na gavana Galerius Maximus, mwakilishi wa serikali ya Dola la Roma.

Jina linatokana na jinsi walivyouawa kwa kutupwa katika shimo la chokaa hai na hivyo kugeuka rundu la vumbi jeupe; tukio hilo ni la kati ya miaka 253-260 [1].

Sifa yao imedumishwa na maandishi ya Agostino wa Hippo na Prudentius.

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yako huadhimishwa tarehe 24 Agosti[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1.   "Massa Candida". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
  2. Under the date 24 August, the "Martyrologium Romanum" records this commemoration: At Carthage, of three hundred holy martyrs in the time of Valerian and Gallienus. Among other torments, the governor ordering a limekiln to be lighted and live coals with incense to be set near by, said to these confessors of the Faith: "Choose whether you will offer incense to Jupiter or be thrown down into lime." And they, armed with faith, confessing Christ, the Son of God, with one swift impulse hurled themselves into the fire, where in the fumes of the burning lime, they were reduced to a powder. Hence this band of blessed ones in white raiment have been held worthy of the name, White Mass.