Matias Mulumba Kalemba

Matias Mulumba Kalemba (1836 - Kampala, 30 Mei 1886) ni mfiadini mmojawapo kati ya Wakristo 22 wa Kanisa Katoliki wanaojulikana na kuheshimiwa duniani kote kama Wafiadini wa Uganda.

Hao walikuwa wahudumu wa ikulu ya kabaka wa Buganda Mwanga II (1884 - 1903) ambao waliuawa kati ya tarehe 15 Novemba 1885 na tarehe 27 Januari 1887 kwa sababu ya kumwamini Yesu Kristo baada ya kuhubiriwa Injili na Wamisionari wa Afrika walioandaliwa na kardinali Charles Lavigerie.

Hawa ndio wafiadini wa kwanza wa Kusini kwa Sahara kuheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu.

Hapo awali Mulumba (yaani "Mwenye Nguvu") alijiunga na Uislamu, lakini baadaye alibatizwa na, kisha kuacha kazi ya hakimu, alijitahidi kueneza imani ya Kikristo. Kwa ajili hiyo aliteswa na mfalme na hatimaye alimkabidhi Mungu roho yake huku akikosa faraja yoyote ya kibinadamu.

Pamoja na wenzake alitangazwa na Papa Benedikto XV kuwa wenye heri tarehe 6 Juni 1920, halafu na Papa Paulo VI kuwa mtakatifu tarehe 18 Oktoba 1964 huko Roma.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 3 Juni, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 30 Mei[1].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.