Matthijs de Ligt

Mchezaji wa shirikisho la mpira uholanzi

Matthijs de Ligt (alizaliwa 12 Agosti 1999) ni mchezaji wa soka anayechezea timu ya taifa ya Uholanzi na klabu ya Ajax iliyopo nchini humo.

Matthijs de Ligt

Mnamo 21 Septemba 2016, de Ligt alicheza kwa mara ya kwanza katika klabu ya Ajax katika mchezo wa kikombe dhidi ya Willem II. Alifunga goli katika dakika ya 25, akiwa mchezaji wa pili mdogo aliyewahi baada ya Clarence Seedorf.

Mnamo 24 Mei, akawa mchezaji mdogo zaidi milele akiwa na miaka 17 na siku 285 kucheza Ulaya alipoanza mechi dhidi ya Manchester United katika mwaka wa 2017 katika UEFA Europa League.

Mnamo tarehe 17 Desemba 2018, de Ligt alishinda tuzo ya Golden Boy, kuwa mchezaji mdogo wa kwanza kushinda tuzo hiyo, Mwaka 2017 de Ligt alichezea Uholanzi kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 17, na kumfanya awe mchezaji mdogo zaidi katika timu ya taifa kutokea tena tangu mwaka 1931.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Matthijs de Ligt kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.