Mavanga ni kata ya Wilaya ya Ludewa katika Mkoa wa Njombe, Tanzania. Msimbo wa posta ni 59416.

Kata ya Mavanga
Nchi Tanzania
Mkoa Njombe
Wilaya Ludewa
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 9,738

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 9,738 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,651 [2] walioishi humo.

Katika kata ya Mavanga kuna mazao mbalimbali ya kawaida kama maharage, mahindi, viazi vitamu, ufuta, ndizi, mihogo, miwa, karanga, njugu mawe, kunde, na vinginevyo.

Kata ya Mavanga ina shule za msingi nne na ya Shule ya Sekondari moja. Kata ya Mavanga ina vijiji viwili ambavyo ni Mavanga na Mbugani. Mavanga ni moja kati ya kata ambazo zimepata huduma ya umeme wa maji kutokana na mradi wa Umeme wa Maji (Small Scale Hydro electric Power Plant) kwa ufadhili kutoka Duren Ujerumani chini ya usimamizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Njombe.

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz, uk 210
  2. "Sensa ya 2012, Njombe - Ludewa DC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-16. 
  Kata za Wilaya ya Ludewa - Mkoa wa Njombe - Tanzania  

Ibumi | Iwela | Kilondo | Lifuma | Luana | Lubonde | Ludende | Ludewa | Lugarawa | Luilo | Lumbila | Lupanga | Lupingu | Madilu | Madope | Makonde | Manda | Masasi | Mavanga | Mawengi | Milo | Mkongobaki | Mlangali | Mundindi | Nkomang'ombe | Ruhuhu


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mavanga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.