Mazoezi ya mwili (kwa Kiingereza "physical exercises") ni vitendo vinavyofanywa aghalabu na watu au mtu ili kuuweka mwili katika hali ya afya nzuri na kuwa tayari kwa ajili ya jambo maalumu.

Watu wakikimbia mchakamchaka.
Mazoezi ya viungo

Inafaa uanze mazoezi hayo kwa dakika kumi kama mwili wako haujazoea kufanya mazoezi. Polepole, ongeza wakati huo uwe dakika mia na hamsini.

Mifano ya mazoezi hariri

  1. Kutembea ("jogging" kwa Kiingereza)
  2. Kucheza dansi
  3. Kukwea milima
  4. Kuendesha baiskeli
  5. Kuogelea
  6. Kucheza tennis, basketball au football
  7. Kucheza na kamba ya battle rope
  8. Mazoezi ya mwili mzima ya machine za kisasa za mtetemo[1][2][3]

umuhimu wa mazoezi hariri

Mazoezi yana umuhimu sana katika mwili wa binadamu kwa kuwa:

  1. mazoezi kama vile kunyanyua vyuma huimarisha mifupa na misuli
  2. mazoezi huboresha upatikanaji wa hewa na virutubishi kwenye seli za mwili
  3. mazoezi husaidia kuzuia maradhi na magonjwa kama vile saratani na pia usizeeke mapema
  4. mazoezi huboresha mfumo wa kupata usingizi
  5. mazoezi huongeza nguvu mwilini.
  6. Mazoezi hupunguza uwezekano wa kupata maradhi makali kama vile shinikizo la damu, bolisukari
  7. Mazoezi huweza kupunguza uzani wa kupindukia kwa wale ambao wako katika hali hii.

Kwa sababu hizo tunashauriwa kufanya mazoezi ili miili yetu iwe imara na yenye afya nzuri. Tunashauriwa tufanye mazoezi kila asubuhi na mchana, kwa kunyoosha viungo kwa namna mbalimbali, ili kupunguza mawazo, na pia ili kuuweka mwili sawa, kuongezeka kwa ukuaji, kuzuia kuzeeka, kuimarisha misuli na mfumo wa moyo, kuvumilia ujuzi wa mashindano, kupoteza uzito, na pia kufurahia.

Kujilinda wakati wa mazoezi hariri

  • Fanya mazoezi mepesi kabla na baada ya zoezi lako kuu ili mwili upate joto kwanza na uweze kutulia baada ya mazoezi.
  • Kunywa maji mengi

Tanbihi hariri

  1. Ritzmann, Ramona; Kramer, Andreas; Bernhardt, Sascha; Gollhofer, Albert (2014-02-26). "Whole Body Vibration Training - Improving Balance Control and Muscle Endurance". PLOS ONE (in English) 9 (2): e89905. ISSN 1932-6203. PMC PMC3935964 Check |pmc= value (help). PMID 24587114. doi:10.1371/journal.pone.0089905. 
  2. Laskowski, Edward R.. Is whole-body vibration an effective workout? (en-US). Iliwekwa mnamo 7 July 2018.
  3. Sudeshna Dey. KnockYourVibe: Frequency of vibration machines and its impact on the human body (en-US). KnockYourVibe - Learn about Whole Body Vibration Machines. Iliwekwa mnamo 7 July 2018.

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mazoezi ya mwili kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.