Mbwana Samatta

Mchezaji wa chama cha soka Tanzania

Mbwana Ally Samatta (alizaliwa 23 Disemba 1992), ni mchezaji wa mpira wa miguu wa Tanzania katika klabu ya Feberbahce ya nchini Uturuki [1]. Mbwana ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na kabla ya kuhamia klabu ya Feberbahce (Uturuki) alikuwa akichezea timu ya Aston Villa ya nchini Uingereza[2].

Mbwana Samatta
Maelezo binafsi
Jina kamiliMbwana Aly Samatta
tarehe ya kuzaliwa23 Desemba 1992 (1992-12-23) (umri 31)
mahali pa kuzaliwaDar es Salaam, Tanzania
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasaFenerbahce
Youth career
2008–2010African Lyon
Senior career*
MiakaTimuApps(Gls)
2010–2011Simba
2011–2016TP Mazembe
2016–2020K.R.C Genk
2020– 2020Aston Villa
Timu ya Taifa ya Kandanda
Tanzania17(6)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only.

† Appearances (Goals).

‡ National team caps and goals correct as of 24 March 2013

Samatta alianza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya African Lyon mwaka 2008 ya nchini Tanzania. Alisajiliwa na klabu ya Simba S.C. mwaka 2010, ambapo alicheza katika nusu msimu tu kabla ya kujiunga na klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Alicheza kwa miaka mitano ndani ya TP Mazembe na kujijengea nafasi katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.

Mwaka 2015, alishinda taji la mchezaji bora wa mwaka wa Afrika, na kumaliza msimu akiwa mfungaji bora wa mashindano ya klabu bingwa Afrika (Ligi ya Mabingwa Afrika) na kuisaidia klabu yake kushinda taji hilo.

Samatta alijiunga na klabu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji mnamo januari 2016, aliisaidia kufuzu michuano ya Ulaya maarufu kama Europa Ligi na kushinda taji la ligi ya Ubelgiji (Belgian Jupiler Ligi mwaka 2019. Alimaliza msimu akiwa mfungaji bora wa ligi hiyo akashinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Ubelgiji (Ebony Shoe award)[3].

Kazi hariri

Samatta alikua mchezaji muhimu wa TP Mazembe waliposhinda taji la klabu bingwa Afrika mwaka 2015 (2015 CAF Champions Ligi), akifunga jumla ya magoli saba na kumaliza akiwa mfungaji bora.[4]

Mnamo Januari 2016, aliposhinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kutokea Afrika ya Mashariki kutwaa tuzo hiyo. Katika ugawaji wa tuzo hizo uliofanyika jijini Abuja, Nigeria, tarehe 7 Januari 2016, Samatta alikusanya jumla ya alama 127, akimzidi mchezaji mwenzake Robert Kidiaba mlinda lango wa TP Mazembe na timu ya taifa ya DR Congo aliyepata alama 88. Baghdad Bounedjah raia wa Algeria alishika nafasi ya tatu akiwa na alama 63.[5] Katika mchezo dhidi ya Moghreb Tétouan ya Moroko, Samatta alifunga magoli matatu kwa mpigo (hat-trick) yaliyowafanya wasonge hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa Afrika. Magoli hayo yanakumbukwa sana katika historia ya klabu ya TP Mazembe.[6]

Muda mfupi baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, alijiunga na klabu ya K.R.C. Genk kwa mkataba wa miaka minne na nusu.[7] Tarehe 23 Agosti 2018 Samatta alifunga goli tatu kwa mpigo(hat-trick) dhidi ya Brøndby IFkwenye mashindano ya Ulaya maarufu kwa jina la Europa Ligi walfanikiwa kupata ushindi wa goli 5–2.[8]

Mei 2019 aliishinda tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Ubelgiji (Ebony Shoe).

Maisha binafsi hariri

Mbwana Samatta ni Mndengereko kutoka Kibiti kwa kabila. Katika maisha ya imani ni Muislamu.[9]

Takwimu za michezo hariri

Klabu hariri

Michezo na magoli ya klabu, Msimu na mashindano
Klabu Msimu Ligi Cup Kombe la ligi Ya Bara Mengineyo Jumla Ref.
Ushindani Michezo Magoli Michezo Magoli Michezo Magoli Michezo Magoli Michezo Magoli Michezo Magoli
Simba S.C. 2010–11 Ligi Kuu Tanzania Bara 25 13 Kigezo:Efn 2 25 15 [10][11]
TP Mazembe 2011 Linafoot 8 2 8 2 [10][11]
2012 29 23 9 6 37 29 [10][11]
2013 37 20 5Kigezo:Efn 5 42 25 [10][11]
2013–14 29 15 8 4 37 19 [10][11]
2014–15 6 4 6 4 [11]
2015–16 6 4 6 4 [11]
Jumla 103 60 0 0 33 23 0 0 136 83
K.R.C. Genk Ligi kuu ya Ubelgiji 6 2 0 0 12Kigezo:Efn 3 18 5 [12]
2016–17 27 10 4 2 18 5 10Kigezo:Efn 3 59 20 [12]
2017–18 20 4 4 0 11Kigezo:Efn 4 35 8 [12]
2018–19 28 20 1 0 12 9 10Kigezo:Efn 3 51 32 [12]
Jumla 81 36 9 2 0 0 30 14 43 13 163 65
Jumla maisha ya soka 209 109 9 2 0 0 63 39 43 13 324 163

Kimataifa hariri

[10]

Taifa Stars
Mwaka Michezo Magoli
2011 9 2
2012 4 0
2013 10 6
2014 3 1
2015 7 2
2016 4 1
2017 3 3
2018 5 2
2019 6 1
Total 51 18

Magoli Kimataifa hariri

Goli Tarehe Uwanja Mpinzani Alama Matokeo Mashindano
1. 26 Machi 2011 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Tanzania   Jamhuri ya Afrika ya Kati 2–1 2–1 kufuzu AFCON 2012
2. 3 Septemba 2011   Algeria 1–0 1–1
3. 11 Januari 2013 Uwanja wa Adis ababa, Addis Ababa, Ethiopia   Ethiopia 1–1 1–2 Mchezo wa Kirafiki
4. 6 Februari 2013 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam   Kamerun 1–0 1–0
5. 24 Machi 2013   Moroko 2–0 3–1 kufuzu fainali za kombe la dunia 2014
6. 3–0
7. 4 Disemba 2013 Uwanja wa Afraha, Nakuru, Kenya   Burundi 1–0 1–0 hatua ya makundi mashindano ya CECAFA 2013
8. 12 Disemba 2013 uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya   Zambia 1–1 1–1 mashindano ya CECAFA hatua ya mtoano 2013
9. 3 Agosti 2014 uwanja wa Estádio do Zimpeto, Maputo, Msumbiji   Msumbiji 1–1 1–2 Kufuzu AFCON 2015
10. 7 Oktoba 2015 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania   Malawi 1–0 2–0 kufuzu fainali za kombe la dunia 2018 hatua ya kwanza
11. 14 Novemba 2015   Algeria 2–0 2–2 kufuzu fainali za kombe la dunia 2018 – hatua ya pili
12. 23 Machi 2016 uwanja wa Stade Omnisports Idriss Mahamat Ouya, N'Djamena, Chad   Chad 1–0 1–0 kufuzu AFCON 2017 hatua ya makundi
13. 25 Machi 2017 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania   Botswana 1–0 2–0 Mchezo wa kirafiki
14. 2–0
15. 10 Juni 2017   Lesotho 1–0 1–1 kufuzu AFCON 2019 Kundi L
16. 27 Machi 2018   Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo 1–0 2–0 Mchezo wa kirafiki
17. 16 Oktoba 2018   Cabo Verde 2–0 2–0 kufuzu AFCON 2019
18. 27 Juni 2019 uwanja wa 30 June Stadium, Cairo, Misri   Kenya 2–1 2–3 AFCON 2019 Kundi C
19. 8 Septemba 2019 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Tanzania   Burundi 1–0 1–1 (3–0 mikwaju ya penalti) kufuzu michano ya kombe la dunia 2022 hatua ya kwanza

Heshima hariri

TP Mazembe[13]

Genk

  • Ligi kuu ya Ubelgiji: msimu wa 2018–19[16]
  • Belgian Super Cup: michuano ya pili ya Ubelgiji 2019[17]

Binafsi

  • Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika: 2015
  • Timu yam waka ya CAF: 2015[18]
  • Mfungaji bora ligi ya mabingwa Afrika: 2015[4]
  • Mchezaji bora ligi ya Ubelgiji: 2019[3]
  • Mfungaji bora ligi ya Ubelgiji: msimu wa 2018-19[17]

Marejeo hariri

  1. Mbwana Samatta Fenerbahçemizde (25 September 2020).
  2. https://www.thecitizen.co.tz/news/Sports/Mbwana-Samatta-joins-Fenerbahce-on-loan/1840572-5627064-au6qg8/index.html
  3. 3.0 3.1 Barrie, Mohamed Fajah (7 May 2019). Tanzania's Mbwana Samatta wins Belgium's Ebony Shoe award. Iliwekwa mnamo 28 August 2019.
  4. 4.0 4.1 "TP Mazembe beat USM Alger to win African Champions Ligi", BBC Sport, 8 November 2015. Retrieved on 25 August 2016. 
  5. Tanzania's Samatta is African Player of the Year Based in Africa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-01-27. Iliwekwa mnamo 8 January 2016.
  6. "Mazembe's Tanzania star Samatta harbours European hopes", BBC Sport, 20 September 2015. Retrieved on 7 January 2018. 
  7. "Mbwana Samatta signs for Belgian side Genk", BBC Sport, 29 January 2016. Retrieved on 25 August 2016. 
  8. Tosin Morakinyo (23 August 2018). Mbwana Samatta’s hat-trick fires Genk past Broendby IF. Goal.com. Iliwekwa mnamo 4 September 2018.
  9. Picha: Mbwana Samatta atua Mecca kufanya Umrah (Swahili) (30 May 2018). Iliwekwa mnamo 28 September 2019.
  10. 10.0 10.1 10.2 10.3 10.4 10.5 Mbwana Aly Samata. Iliwekwa mnamo 5 March 2019.
  11. 11.0 11.1 11.2 11.3 11.4 11.5 11.6 Kigezo:Soccerway
  12. 12.0 12.1 12.2 12.3 Mbwana Samatta » Club matches. Iliwekwa mnamo 20 October 2018.
  13. Mbwana Samatta is carrying Tanzania's torch in Europe. First Touch (3 March 2019). Jalada kutoka ya awali juu ya 2019-07-12. Iliwekwa mnamo 12 July 2019.
  14. Advantage Mazembe in CAF final after away win. CAF (1 November 2015).
  15. Mazembe beat USMA to reach fifth heaven. CAF (8 November 2015).
  16. Tanzania captain Mbwana Samatta linked with move to Middlesbrough. Goal (3 July 2019). Iliwekwa mnamo 12 July 2019.
  17. 17.0 17.1 Landskampioen Genk opent seizoen met Supercup-winst tegen KV Mechelen. Sporza (20 July 2019). Iliwekwa mnamo 21 July 2019.
  18. "Aubameyang, Samatta Rule Africa", CAF, January 7, 2016. Retrieved on January 7, 2016. 
  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mbwana Samatta kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.