Mcheduara (pia silinda; kwa Kiingereza: cylinder) ni gimba la kijiometri linalofanana na kopo au kipande cha pipa. Hivyo jina lake linaeleza ni mche wenye umbo la duara au mviringo. Gimba la mcheduara linapakanwa na miduara bapa miwili inayokaa sambamba na kuwa vitako vyake.

Kopo hili lina umbo la mcheduara.
Mcheduara mraba na mshadhari.
Mcheduara mraba.

Kihisabati mcheduara unaweza kufafanuliwa pia kama uso ambao ni jumla ya nukta zote zenye umbali sawa na mstari ulio katikati yake unaojulikana kama "mhimili" wake. Hii ni bila kitako.

Kutokana na ufafanuzi huo gimba la mchemraba ni umbo thabiti uliomo ndani ya uso huo ukipakanwa na vitako viwili bapa sambamba.

  • Kama vitako vinakaa kwa pembemraba juu ya mhimili, mcheduara huitwa mraba.
  • Kama vitako vinakaa kwa pembe tofauti, tunapata mcheduara mshadhari.

Mcheduara mraba huwa na

  • mjao V = π r 2 h
  • eneo la uso bila bapa zinazopakana M = 2 π r h
  • eneo la uso wote E = 2 π r 2 + 2 π r h
Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mcheduara kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.