Mdudu Mabawa-vigamba

Mdudu mabawa-vigamba
Kipepeo mikia-mbayuwayu mweupe (Papilio dardanus)
Kipepeo mikia-mbayuwayu mweupe (Papilio dardanus)
Bundo lake
Bundo lake
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Lepidoptera (Wadudu wenye mabawa yaliyo na vigamba juu yao)
Linnaeus, 1758
Ngazi za chini

Nusuoda 4:

Wadudu mabawa-vigamba ni wadudu wadogo hadi wakubwa wa oda Lepidoptera katika nusungeli Pterygota (wenye mabawa). Jina ni tafsiri ya jina la kisayansi. Wadudu hawa wanajulikana kama vipepeo na nondo.

Wadudu hawa wana mabawa kama viwambo, isipokuwa spishi kadhaa ambazo zina mabawa yaliyopunguka au hazina mabawa kabisa. Kinyume na wadudu mabawa-viwambo kwa kawaida mabawa yao yamefunikwa kwa vigamba ambavyo kweli ni manyoya yaliyofanyika kuwa bapa. Lakini mabawa ya spishi kadhaa yana sehemu bila vigamba zilizo nyangavu kwa hivyo (k.m. Nondo mkia-mshale mwangavu).

Sehemu za kinywa za spishi nyingi zimetoholewa kuwa mrija mrefu sana unaoitwa ulimi au proboski. Mrija huo hutumiwa kufyonza mbochi au viowevu vingine. Lakini spishi za Zeugloptera bado zina sehemu za kutafuna kama ndugu wao wa oda Trichoptera (Wadudu mabawa-manyoya).

Wachanga wa vipepeo na nondo huitwa viwavi. Hawafanani na wapevu kwa sababu hawana mabawa, wana sehemu za kinywa za kutafuna na wana miguu bandia kwenye fumbatio licha ya miguu sita ya kweli kwenye toraksi. Kwa kawaida viwavi hula majani ya mimea na mara nyingi shina pia na pengine hata matunda. Spishi fulani za viwavi hula wadudu wengine na nyingine ni vidusia.

Spishi kadhaa za Afrika ya Mashariki hariri

Mwainisho hariri

Picha hariri

  Makala hii kuhusu mdudu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mdudu Mabawa-vigamba kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.