Mfalme Amon (664 KK641 KK) alikuwa mfalme wa 15 wa Yuda (643 KK – 641 KK au 642 KK - 640 KK) aliyeendeleza ibada za miungu ili kufuata dini za mataifa makuu ya wakati huo, hata kutumia Hekalu la Yerusalemu. Kwa kwenda kinyume cha imani ya Israeli hata aliuawa na watumishi wake (2 Wafalme 21:18-26; 2 Mambo ya Nyakati 33:22).

Mfalme Amon.

Familia hariri

Mwana wa mfalme Manase, anayetajwa na Biblia kama mmojawapo kati ya wafalme waovu zaidi wa ukoo wa Daudi kinyume cha uaminifu wa baba yake Hezekia [1], na Meshullemet, alirithi utawala akiwa kijana wa miaka 22 akatawala miaka 2 tu.

Mfalme Amoni alimuoa Jedidah, nao walikuwa na mwana aliyeitwa Yosia.

Anatajwa pia katika Injili ya Mathayo (1:10) kati ya mababu wa Yesu.

Tanbihi hariri

  1. II Kings states that Amon "did that which was evil in the sight of Yahweh, as did Manasseh his father. And he walked in all the way that his father walked in, and served the idols that his father served, and worshipped them."

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mfalme Amoni kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.