Mikese ni kata ya Wilaya ya Morogoro Vijijini katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania, yenye Postikodi nambs 67206.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 23,637 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 15,569 [2] walioishi humo.

Kata ya Mikese ina shule za sekondari takriban tano ambazo ni za serikali, pia kuna hospitali nne za serikali.

Ndani ya kata hiyo kuna pia shule ya mtu binafsi inayojulikana kwa jina la Herberth Wallbrecher yenye maendeleo mazuri sana kitaaluma. Shule hii ipo chini ya Kanisa Katoliki ambapo mwanafunzi analelewa kulingana na maadili ya kidini. Anaruhusiwa kukaa bweni kuanzia darasa la tatu mpaka la saba pia kuwa mwanafunzi wa kutwa.

Marejeo hariri

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. Sensa ya 2012, Morogoro - Morogoro DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2015-03-22.
  Kata za Wilaya ya Morogoro Vijijini - Mkoa wa Morogoro - Tanzania  

Bungu | Bwakira Chini | Bwakira Juu | Gwata | Kasanga | Kibogwa | Kibuko | Kibungo | Kidugalo | Kinole | Kiroka | Kisaki | Kisemu | Kolero | Konde | Lundi | Matuli | Mikese | Mkambalani | Mkulazi | Mkuyuni | Mngazi | Mtombozi | Mvuha | Ngerengere | Selembala | Singisa | Tawa | Tegetero | Tomondo | Tununguo


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Morogoro bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mikese kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa na viongozi wa sasa maana wanabadilika haraka mno.