Milima ya Uluguru ni safu ya milima katika Tanzania mashariki, km 200 hivi kutoka Bahari ya Hindi. Ni sehemu ya Milima ya Tao la Mashariki (pamoja na Milima ya Taita nchini Kenya, Milima ya Upare, Milima ya Usambara, Milima ya Unguu, Milima ya Rubeho, Milima ya Ukaguru, Milima ya Udzungwa, Milima ya Uvidunda na Milima ya Mahenge).

Mashamba ya katani nje kidogo ya Morogoro. Milima ya Uluguru inaweza kuonekana nyuma
milima uluguru
Mandhari ya milima ya Uluguru.
Mlima wa Uluguru nyuma ya Morogoro.
Chemchemi karibu na Kinole.
Mashamba ya katani karibu na mji wa Morogoro. Milima ya Uluguru inaonekana kwa nyuma.

Jina limetokana na lile la kabila la Waluguru ambao ndio wenyeji wa eneo hilo.[1] Wakazi wote wa milimani huko ni 151,000.

Milima ya Uluguru ni makazi pekee ya spishi zaidi ya 100 ya mimea, 2 za ndege, 2 za mamalia, 4 za reptilia na 6 za amphibia.

Miinuko ya juu zaidi ni mlima Mtingire na mlima Kimhandu, yote miwili inafikia kimo cha mita 2650 juu ya usawa wa bahari[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. "Tanzania Tourist Board". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-10-09. Iliwekwa mnamo 2018-03-02. 
  2. "Uluguru". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-28. Iliwekwa mnamo 2018-03-02. 

7°10′S 37°40′E / 7.167°S 37.667°E / -7.167; 37.667