Milima ya Zagros (kwa Kifarsi: کوه‌های زاگرس kuh-haye zagros) ni safu ya milima katika magharibi na kusini-magharibi nchini Iran ikienea pia katika Iraki na Uturuki.

Maeneo ya milima ya Zagros nchini Iran (mstari mwekundu)
Mlima Dena, kilele cha juu katika milima ya Zagros.

Urefu wake ni mnamo kilomita 1,500. Safu inaanza kaskazini-magharibi mwa Iran, ikifuata mpaka wa magharibi wa nchi hiyo halafu pwani ya Ghuba ya Uajemi upande wa kusini, ikiishia kwenye mlangobahari wa Hormuz.

Miinuko ya juu zaidi katika Milima ya Zagros ni Zard Kuh (mita 4,548) na mlima Dena (m 4,359).

Eneo la Zagros ni sehemu muhimu ya uzalishaji wa mafuta ya petroli.

Marejeo hariri

Tovuti za Nje hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Milima ya Zagros kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.