Mshororo ni kila mstari uliopo ndani ya beti za shairi.

Idadi ya mishororo katika shairi ndio hutumika katika kutambua na kujua aina ya shairi[1]. Kanuni hiyo hutumika sana katika mashairi ya kimapokeo. Mara nyingi mishororo huanza kwa kuwa na kipande kimoja katika mstari, vipande viwili, vipande vitatu, na vipande vinne.

Washairi wengi wamekua wakiandika mshororo wenye vipande viwili kwa mashairi ya kawaida na wachache sana hujaribu kuandika mashairi yenye vipande viwili katika mshororo.

Kila mshororo huwa na majina yake kwa mashairi yenye mishororo minne ambayo hujulikana kama Tarbia.

Mshororo wa kwanza huitwa Mwanzo.

Mshororo wa pili huitwa Mloto.

Mshororo wa tatu huitwa Mleo.

Mshororo wa nne huitwa Kituo. Iwapo mshororo wa mwisho katika ubeti utajirudiarudia, basi mshororo huo utabadilika jina kutoka kituo na kuitwa Kibwagizo.

Tanbihi hariri

  1. Aina za Mashairi | Paneli la Kiswahili. swa.gafkosoft.com. Iliwekwa mnamo 2020-01-27.
  Makala hii kuhusu mambo ya fasihi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mshororo kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.