Mtangawizi
Mitangawizi
Mitangawizi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Monocots (Mimea ambayo mche wao una jani moja)
(bila tabaka): Commelinids (Mimea kama jaja)
Oda: Zingiberales (Mimea kama mtangawizi)
Familia: Zingiberaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mtangawizi)
Jenasi: Zingiber
Mill.
Spishi: Z. officinale
Roscoe

Mtangawizi (jina la kisayansi: Zingiber officinale) ni mmea wa familia Zingiberaceae katika ngeli ya Monokotiledoni. Mizizi yake yanayoitwa tangawizi hutumika kama kiungo katika chakula na unga wake hutumika katika vinywaji na katika chakula pia.

Matumizi ya tangawizi hariri

Tangawizi (kwa Kilatini zingiberis rhizoma; kwa Kiingereza: ginger (root)) ina umbo kama la mzizi wa manjano na yote miwili hutumika kama viungo katika chakula.

Tangawizi huwa na utomvu wenye mafuta na kampaundi zinazofanya ukali wake. Utafiti wa kisasa umegundua tagawizi inaweza kusaidia kwenye matatizo ya utumbo na kuzuia kutapika[1].

Imetazamiwa tangawizi inapunguza maumivu ya viungo vilivyoathiriwa na rumatizimu na athritisi[2].

Picha hariri

Marejeo hariri

  1. Effects of ginger on motion sickness and gastric slow-wave dysrhythmias induced by circular vection.
  2. JK. Kim, Y. Kim, KM. Na, YJ. Surh, TY. Kim: [6-Gingerol prevents UVB-induced ROS production and COX-2 expression in vitro and in vivo]. In: Free Radic Res. 2007, 41 (5), pp. 603–614
  Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtangawizi kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.