Mto Osun ni mto nchini Nigeria ambao chanzo chake kinapatikana jimbo la Ekiti na umepita kusini mwa Yorubaland ya kusini magharibi mwa Nigeria kuingia mjini Lagos Lagoon na kuishia Ghuba ya Guinea katika ya Atlantiki. [1]

Chanzo cha mto Osun huko Oshogbo.

Ni mojawapo ya mito kadhaa iliyoainishwa katika hadithi za kienyeji kuwa wanawake ambao waligeuka kuwa maji yanayotiririka baada ya tukio fulani lenye kuogofya kuwaogopa au kuwakasirisha.

Mto Osun una urefu wa kilometa 267. Mto huo ulipewa jina la Oṣun, jina lililotokana na jina la miungu la Osun au Oshun iliyokuwa maarufu katika jamii ya Wayoruba.[2]

Ibada ya jadi katika Shimoni la Ọṣun karibu na mto wa Ọṣun huko Osogbo imekuwa maarufu kama Hija na kivutio muhimu cha watalii, ikivuta watu kutoka kote nchini Nigeria na nje ya nchi kwa sherehe ya kila mwaka mwezi Agosti.

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. https://www.geonames.org/2325587/river-osun.html
  2. "Osun river", Wikipedia (in English), 2019-08-19, retrieved 2020-02-07 
  Makala hii kuhusu maeneo ya Nigeria bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Osun kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.