Mwaka wa Lugha wa Kimataifa

Mwaka wa 2008 umetangazwa kuwa Mwaka wa Lugha wa Kimataifa na Umoja wa Mataifa katika azimio lililopitishwa tarehe 16 Mei 2007.[1][2]

Mwaka huo, mpango wake ni kujadili mambo ya wingi wa lugha, haki za lugha zote, na mazingira ya kutumia lugha tofauti. Azimio la kutangaza mwaka huo linataja pia shida za lugha ndani ya Umoja wa Mataifa wenyewe.[3]

Shirika la UNESCO limepewa kazi ya kupanga utekelezaji wa mwaka huo, na wameufungulia rasmi kwenye Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Mama, tarehe 21 Februari 2008.[4]

Viungo vya Nje hariri

Marejeo hariri


  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwaka wa Lugha wa Kimataifa kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.