Nabii Hagai (kwa Kiebrania חַגַּי, Ḥaggay au "Hag-i", yaani Sikukuu yangu; kwa Kigiriki: Ἀγγαῖος; kwa Kilatini Aggeus) ni mmojawapo kati ya manabii wa Israeli, aliyetoa ujumbe wake miezi ya mwisho ya mwaka 520 KK tu, akihimiza pamoja na nabii Zekaria ujenzi mpya wa hekalu la Yerusalemu baada ya Wayahudi kurudi toka uhamisho wa Babeli.

Picha takatifu ya Kirusi ya Hagai, karne ya 18 (katika ukuta wa picha wa monasteri ya Kizhi, Karelia, Russia).

Hatimaye kazi hiyo ilikamilika na hekalu likatabarukiwa mwaka 515 KK.

Maandishi hariri

Kitabu chake ni kati ya Manabii Wadogo 12 wa Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania), kwa hiyo pia kinapatikana katika Agano la Kale, sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.

Heshima baada ya kifo hariri

Tangu kale Hagai anaheshimiwa kama mtakatifu, hasa tarehe 16 Desemba[1][2] lakini pia 29 Desemba, au 4 Julai au 16 Julai au 31 Julai.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Carroll Stuhlmueller, Haggai and Zechariah: Rebuilding With Hope. Edinburgh: The Handsel Press Ltd., 1988. ISBN 978-0-905312-75-0.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nabii Hagai kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.