Wilaya ya Nachingwea

(Elekezwa kutoka Nachingwea)

Wilaya ya Nachingwea ni kati ya wilaya za Mkoa wa Lindi, yenye postikodi inayoanzia namba 653.

Mahali pa Nachingwea (kijani cheusi) katika mkoa wa Lindi (kijani) na Tanzania kwa jumla.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa wilaya ya Nachingwea Mjini walihesabiwa 233,655 [1]. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 162,081 [2].

Wilaya hii imepakana na wilaya za Ruangwa upande wa kaskazini, Lindi Vijijini upande wa mashariki, halafu na mikoa ya Mtwara na Ruvuma upande wa kusini.

Nachingwea kuna hospitali, Chuo cha Ualimu, shule za sekondari 3 na za msingi 81 wilayani.

Eneo hili lilikuwa sehemu ya mradi wa karanga wakati wa ukoloni wa Uingereza.

Kuna madini ya nikeli katika Nachingwea na kampuni ya IMX Resources NL (zamani Goldstream Mining) kutoka Australia imeanzisha kampuni "Continental Nickel" ya kuchimba nikeli hiyo lakini hadi mwaka 2008 bado ilikuwa ikitafuta pesa kwenye soko la hisa la Kanada.

Asili ya Nachingwea hariri

Neno Nachingwea asili yake ni mti mmoja uliokuwa ukiitwa Ngwea. Wakazi wa makao makuu ya wilaya ya Nachingwea, wakati huo Ruponda, walikuwa wakienda kuchota maji chini ya mti wa Ngwea, kwa hiyo walikuwa wakisema Nachi Ngwea wakimaanisha naenda kwenye Ngwea, maana yake naenda kuchota maji kwenye ngwea. Ndipo jina hilo likashika kasi na kuwa Nachingwea ya leo.

Viungo vya Nje hariri

Marejeo hariri

  Kata za Wilaya ya Nachingwea - Mkoa wa Lindi - Tanzania  

Boma | Chiola | Chiumbati Shuleni | Kiegei | Kilimanihewa | Kilimarondo | Kipara Mnero | Kipara Mtua | Lionja | Marambo | Matekwe | Mbondo | Mchonda | Mitumbati | Mkoka | Mkotokuyana | Mnero Miembeni | Mnero Ngongo | Mpiruka | Mtua | Nachingwea Mjini | Naipanga | Naipingo | Namapwia | Namatula | Nambambo | Namikango | Nang'ondo | Nangowe | Nditi | Ndomoni | Ngunichile | Raha leo | Ruponda | Stesheni | Ugawaji


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Lindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Nachingwea kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.