Nauli ni ada inayolipwa na abiria kwa matumizi ya chombo cha usafiri wa umma kama vile reli, basi, teksi, ndege, bodaboda, meli n.k.

Muundo wa nauli ni mfumo uliowekwa kuamua ni kiasi gani kinachopaswa kulipwa na abiria wa kila aina wanaotumia usafiri fulani wakati wowote.

Nauli inayolipwa ni mchango kwa gharama za uendeshaji wa mfumo wa usafirishaji unaohusika, ama kisehemu (jinsi ilivyo kawaida na mifumo inayoungwa mkono na umma) au jumla.

Katika mifumo mingi ya usafiri abiria hukata tiketi kabla ya kuanza safari inayolipa gharama hadi kufika mwisho wa safari yake. Nauli inaweza kuwa kwa bei moja kwa matumizi ya usafiri bila kujali umbali, jinsi ilivyo kawaida katika daladala na matatu kwenye miji ya Afrika ya Mashariki[1], au inaweza kuwa tofauti kulingana na umbali wa safari jinsi ilivyo katika huduma za reli na za ndege.

Wakati wa kutumia usafiri wa pekee kama teksi, nauli inaamuliwa mara nyingi baada ya safari kulingana na umbali na muda wa safari.

Katika mifumo sahili kuna kondakta anayekusanya pesa[2] ndani ya chombo cha usafiri, mara nyingi kwa kutoa tiketi kama ushuhuda wa malipo na pia kama risiti. Risiti ni nyaraka inayokubali au kuthibitisha kuwa malipo yamefanyika kwa ajili ya bidhaa au huduma fulani.

Nauli za adhabu ni nauli zinazotozwa kwa abiria wasio na tiketi halali. Nauli za adhabu pia hutozwa kwa dereva wa daladala wenye kosa au wasiofuata sheria na masharti ya njia.

Marejeo hariri

  1. linganisha pia mfano wa Los Angeles, "Fares". Los Angeles County Metropolitan Transportation Authority. Iliwekwa mnamo June 5, 2019.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. Jifunze kuhusu bei za nauli, Fare prices. Fare Prices lilihaririwa mnamo Februari 1, 2023.
  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nauli kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.