Nestori (kwa Kigiriki Νεστόριος, Nestorios; Germanicia, (leo nchini Uturuki) 386 hivi – al-Khargah, Misri, 450[1]) alikuwa mmonaki na mwanateolojia aliyefikia kuwa Patriarki wa Konstantinopoli (leo Istanbul) tangu tarehe 10 Aprili 428 hadi Agosti 431, ambapo kaisari Theodosius II alithibitisha uamuzi dhidi yake uliopitishwa na Mtaguso wa Efeso tarehe 22 Juni.

Nestori kadiri ya Romeyn de Hooghe (1688)

Kwa kukataa jina lililozoeleka la Θεοτόκος, Theotokos, "Mama wa Mungu", kwa Bikira Maria, alisababisha mabishano makubwa na hatimaye mafarakano kuhusu fumbo la Yesu Kristo.

Hasa Sirili wa Aleksandria alimpinga vikali kwa kudai haamini umungu wa Yesu, ingawa mwenyewe alizidi kujitetea hadi kifo chake kwamba anashika imani sahihi.

Anaheshimiwa na Kanisa la Asiria kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 25 Oktoba.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Nestorius Archived 7 Desemba 2017 at the Wayback Machine. Ecumenical Patriarchate

Vyanzo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.