Ngudu ni kata ya Wilaya ya Kwimba katika Mkoa wa Mwanza, Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 27,630 waishio humo.[1]

Msimbo wa posta ni 33801.

Ni moja kati ya kata zinazokua kwa kasi kubwa ndani ya Wilaya ya Kwimba, ambayo ni wilaya kubwa mkoani Mwanza.

Kata ya Ngudu ndiyo inayoongoza katika maendeleo ukiilinganisha na kata nyingine wilayani Kwimba.

Wakazi wa kata ya Ngudu, wengi wao hupendelea chakula aina ya michembe ambapo huweza kusaidia wakati wa uhaba wa chakula.

Uchumi hariri

Kata ya Ngudu inategemea kwa kiasi kikubwa ufugaji wa wanyama kama vile mbuzi, ng'ombe pamoja na kondoo, lakini pia kwa kiasi kikubwa wakazi wa kata ya Ngudu hujihusisha katika kilimo cha jembe la mkono.

Mazao yanayolimwa katika kata ya Ngudu ni kama vile mpunga, mahindi pamoja na viazi vitamu.

Kilimo hiki kwa kiasi kikubwa hutumia jembe la mkono katika kuinua uchumi wa kata.

Marejeo hariri

  Kata za Wilaya ya Kwimba - Mkoa wa Mwanza - Tanzania  

Bugando | Bungulwa | Bupamwa | Fukalo | Hungumalwa | Igongwa | Ilula | Iseni | Kikubiji | Lyoma | Maligisu | Malya | Mantare | Mhande | Mwabomba | Mwagi | Mwakilyambiti | Mwamala | Mwandu | Mwang'halanga | Mwankulwe | Ng'hundi | Ngudu | Ngulla | Nkalalo | Nyambiti | Nyamilama | Shilembo | Sumve | Walla


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mwanza bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ngudu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.