Nikodemo (kwa Kigiriki Νικόδημος, Nikodemos) alikuwa mwalimu wa Torati wa madhehebu ya Mafarisayo tena mwanabaraza wa Baraza la Israeli katika karne ya 1 BK.

Nikodemo akisaidia kushusha maiti ya Yesu kutoka msalabani (Pietà, sanamu iliyochongwa na Michelangelo).

Anaheshimiwa na Wakristo wengi kama mtakatifu, ingawa sikukuu yake inaadhimishwa katika tarehe tofautitofauti, hasa tarehe 31 Agosti[1].

Nikodemo katika Injili hariri

Anajulikana kwa sababu ya kutajwa mara kadhaa katika Injili ya Yohane,[2] kama mtu aliyevutiwa na Yesu Kristo ingawa aliogopa maneno ya Wayahudi wenzake.

Ndiyo sababu alimtembelea usiku ili kumuuliza maswali ya dini yao bila kujulikana (Yoh 3:1–21).

Baadaye katika baraza alimtetea Yesu kwamba si haki kuhukumu bila kumsikiliza kwanza, lakini alinyamazishwa (Yoh 7:50–51).

Hatimaye alimsaidia Yosefu wa Arimataya kumzika Yesu (Yoh 19:39–42).

Nikodemo katika picha hariri

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Martyrologium Romanum
  2. Driscoll, James F. "Nicodemus." The Catholic Encyclopedia. Vol. 11. New York: Robert Appleton Company, 1911. 13 Dec. 2014.

Marejeo hariri

  • Cornel Heinsdorff: Christus, Nikodemus und die Samaritanerin bei Juvencus. Mit einem Anhang zur lateinischen Evangelienvorlage (= Untersuchungen zur antiken Literatur und Geschichte, Bd.67), Berlin/New York 2003

Viungo vya nje hariri

 
WikiMedia Commons
  Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nikodemo kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.