Njia ni sehemu au eneo wazi jembamba ambalo hutumiwa na watu, wanyama au magari kupita, lakini pia namna au mbinu ya kufanya kazi au kutatua tatizo fulani.

Njia ya milimani huko Wilaya ya Shaharah, Yemen.

Mithali maarufu ya Kiswahili inasema, "Penye nia pana njia".

Katika Ukristo hariri

Yesu alifundisha kufuata njia nyembamba inayopeleka uzimani kuliko ile pana inayofikisha upotevuni (Math 7:13-14).

Zaidi ya hayo, mwenyewe alijitangaza kuwa njia pekee ya kumfikia Baba (Yoh 14:6).

Kadiri ya Matendo ya Mitume, Ukristo uliitwa kwanza "Njia" (22:4).

Tazama pia hariri