Nyanda za juu za Brazil

Nyanda za juu za Brazil (kwa Kireno: Planalto Brasileiro) ni eneo kubwa katika mashariki, kusini na katikati ya Brazil. Eneo lake ni kama theluthi ya nchi yote na sehemu kubwa ya watu wa Brazil (190,755,799; sensa ya 2010) wanaishi katika nyanda za juu au kwenye kanda nyembamba ya pwani iliyopo kati ya bahari na milima hiyo.

Ramani ya nyanda za juu za Brazil
Mji mdogo wa Arcoverde katika nyanda za juu

Mgawanyiko mkubwa hariri

Kwa sababu ya ukubwa na utofauti wao, nyanda za juu za Brazil kwa kawaida hugawanywa katika maeneo makuu matatu:

  • Nyanda za juu za Atlantiki, zinazoenea karibu na pwani ya mashariki ya Brazil, na pamoja na safu kadhaa za milima. Ilikuwa karibu imefunikwa kabisa na msitu wa mvua lakini ni asilimia 7.3 tu iliyobaki.
  • Nyanda za juu za Kusini, zinazoendeleza katika sehemu za kusini na kusini-mashariki mwa nchi. Kuna ardhi yenye rutuba inayojulikana kama "ardhi ya zambarau".
  • Nyanda za juu za Kati, inachukua sehemu za kati za Brazil.

Sehemu ya juu zaidi ya Nyanda za juu za Brazil ni Pico da Bandeira huko Serra do Caparaó, inayofikia mita 2,891 juu ya UB.

  Makala hii kuhusu maeneo ya Brazil bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyanda za juu za Brazil kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.