Nzega Mjini ilikuwa kata ya Wilaya ya Nzega katika Mkoa wa Tabora, Tanzania yenye postikodi namba 45401.

Nzega Mjini
Nzega Mjini is located in Tanzania
Nzega Mjini
Nzega Mjini

Mahali pa Nzega Mjini katika Tanzania

Majiranukta: 4°12′54″S 33°11′7″E / 4.21500°S 33.18528°E / -4.21500; 33.18528
Nchi Tanzania
Mkoa Tabora
Wilaya Nzega
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 34,744

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 34,744 waishio humo.[1] Kwa sasa imegawiwa katika kata mpya kama vile Nzega Mjini Mashariki na Nzega Mjini Magharibi.

Kuna kivutio cha bwawa la Uchama ambapo kuna maji mengi: watu hupenda kwenda kutembelea huko; pia maji hutumika kwa shughuli mbalimbali kama kufulia, kumwagilia bustani, kujengea na kunyweshea ng'ombe kwa kuyachota na kuwapa.

Kuna mnada wa nguo na wanyama siku ya Jumamosi ushirika ambapo Wanyamwezi na watu wengine hukutana na kufanya shughuli ya kununua bidhaa. Kipindi cha mnada ni siku ambayo inavutia sana watu: kuna nyama rosti za mbuzi, kondoo na ng'ombe. Pia kuna vinywaji vingi kama soda, bia na juisi. Watu hupata starehe.

Marejeo hariri

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tabora bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nzega Mjini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.