Omdurman (au: Omdourman, Kar: أم درمان Umm Durmān ) ni mji mkubwa kabisa nchini Sudan kando la mto Nile ikitazama mji mkuu Khartoum. Pamoja na Khartoum na Bahri ni mji mmoja kubwa sana unaounganishwa kwa madaraja kadhaa.

Omdurman
jiji, big city
Jina rasmiأم درمان Hariri
Native labelأم درمان Hariri
NchiSudan Hariri
Located in the administrative territorial entityKhartoum Hariri
Located in time zoneUTC+03:00 Hariri
Coordinate location15°41′1″N 32°27′46″E Hariri
Map
Upande wa soko kwa mji wa Omdurman
Omdurman nchini Sudan
Ramani ya Omdurman pamoja na Khartoum na Bahri
Kaburi la Mahdi mjini Omdurman

Ina wakazi wanaokadiriwa kufikia karibu milioni 3.

Historia hariri

Mji ulianzishwa na Muhammad Ahmad ibn Abd Allah Al-Mahdi mwaka 1885. Baada ya jeshi lake kuteka Khartoum katika vita dhidi ya Misri na gavana yake Gordon Mahdi Muhammad hakutaka kukaa kwenye "mji wa makafiri" akajenga mji mpya wa Omdurman "mji wa waumini" ng'ambo ya mto Nile uliokuwa mji mkuu wa dola la Mahdi 1885 - 1898. Wakati ule Omdurman ilikuwa tayari na wakazi 150,000.

Waingereza walipoteka Sudan mwaka 1898 Omdurman ilirudi nyuma lakini wakati wa miaka ya mwisho wa karne ya 20 ilikua tena kupita Khartoum kutokana na kufika kwa wakimbizi wengi mjini kutoka nchi jirani kama Chad, Eritrea, Ethiopia na Uganda, pia wakimbizi kutoka vita ya Sudan ya Kusini. Wakimbizi hawa walijenga mitaa mikubwa ya vibanda.

Utamaduni na elimu hariri

Omdurman ina vyuo vikuu kadhaa. Kumbukumbu ya kihistoria muhimu ni kaburi la Mahdi.


  Makala hii kuhusu maeneo ya Sudan bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Omdurman kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.