Omikron, yaani "o ndogo" (Ο ο) ni herufi ya 15 katika Alfabeti ya Kigiriki. Inaandikwa kama ο (alama ya kawaida) au Ο (alama kubwa). Zamani za Kigiriki cha Kale ilikuwa pia tarakimu ikiwa alama ya namba 70.

Faili:Omikron uc lc.svg
Alfabeti ya Kigiriki
Herufi za kawaida
Α α Alfa 1 Ν ν Ni 50
Β β Beta 2 Ξ ξ Ksi 60
Γ γ Gamma 3 Ο ο Omikron 70
Δ δ Delta 4 Π π Pi 80
Ε ε Epsilon 5 Ρ ρ Rho 100
Ζ ζ Dzeta 7 Σ σ ς Sigma 200
Η η Eta 8 Τ τ Tau 300
Θ θ Theta 9 Υ υ Ipsilon 400
Ι ι Iota 10 Φ φ Phi 500
Κ κ Kappa 20 Χ χ Khi 600
Λλ Lambda 30 Ψ ψ Psi 700
Μ μ Mi 40 Ω ω Omega 800
Herufi za kihistoria1
Digamma 6 San 90
Stigma 6 Sho 90
Heta 8 Koppa 90
Sampi 900
1 Viungo vya Nje:
Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_Nje

Asili ya omikron ni herufi ya Kifinisia "ayin" . Herufi zilizotokana nayo katika alfabeti zilizofuata Kigiriki ni O katika alfabeti ya Kilatini na katika alfabeti ya Kikirili vilevile.

Matamshi yake yalikuwa "o".

Jinsi ilivyo kawaida kwa herufi mbalimbali za Kigiriki, ο inatumiwa kama kifupisho kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hisabati na fizikia.