Orodha ya Makaizari wa Bizanti

Orodha hii inataja makaizari wa Bizanti kuanzia nasaba ya Theodosius hadi mwisho wa Dola la Roma Mashariki mwaka wa 1453.

Nasaba ya akina Theodosius hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
28 Machi, 364 hadi 9 Agosti, 378 Valens Alikufa kwenye mapigano ya Adrianopoli.
19 Januari, 379 hadi 17 Januari, 395 Theodosius I Alipewa mamlaka katika Mashariki kutoka kwa Flavius Gratianus aliyekuwa Kaizari wa Magharibi.
17 Januari, 395 hadi 1 Mei, 408 Arkadius Mwana wa Theodosius I
1 Mei, 408 hadi 28 Julai, 450 Theodosius II Mwana wa Arkadius
450 hadi 2 Januari, 457 Markian Alipata kuwa Kaizari baada ya kumwoa Pulkeria, dada wa Theodosius II

Nasaba ya Thraki hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
7 Februari, 457 hadi 18 Januari, 474 Leo I Aliteuliwa na jenerali Aspar.
18 Januari, 474 hadi 17 Novemba, 474 Leo II Mjukuu wa Leo I.
17 Novemba, 474 hadi 9 Januari, 475 Zeno Baba yake Leo II.
9 Januari, 475 hadi Agosti 476 Basilisko Shemeji wa Leo I.
Agosti 476 hadi 9 Aprili, 491 Zeno awamu yake ya pili
11 Aprili, 491 hadi 9 Julai, 518 Anastasios I Aliteuliwa na Ariadne, mjane wa Zeno, na kumwoa baadaye.

Nasaba ya akina Justiniani hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
Julai 518 hadi 1 Agosti, 527 Justin I
1 Agosti, 527 hadi 14 Novemba, 565 Justiniani I Mpwa na mrithi wa Justin I
14 Novemba, 565 hadi 5 Oktoba, 578 Justin II Mpwa na mrithi wa Justinian I
5 Oktoba, 578 hadi 14 Agosti, 582 Tiberio II Labda aliuawa kwa sumu.
14 Agosti, 582 hadi Novemba 602 Maurikios Alimwoa binti wa Tiberios II

Bila nasaba hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
Novemba 602 hadi Oktoba 610 Fokas

Nasaba ya akina Heraklios hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
5 Oktoba, 610 hadi 11 Februari, 641 Heraklio
Februari 641 hadi 24 Mei, 641 Konstantino III Mwana wa Heraklios; Kaizari-Mshiriki pamoja na Heraklonas
Februari 641 hadi Septemba 641 Heraklonas Mwana wa Heraklios; Kaizari-Mshiriki pamoja na Konstantino III
641 hadi 15 Septemba, 668 Konstans II Mwana wa Konstantino III
Septemba 668 hadi Septemba 685 Konstantino IV Mwana wa Konstans II
Septemba 685 hadi 695 Justiniani II Mwana wa Konstantino IV
695 hadi 698 Leontios Mnyang'anyi
698 hadi 705 Tiberio III Mnyang'anyi
705 hadi Desemba 711 Justiniani II awamu yake ya pili

Bila nasaba hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
Desemba 711 hadi 3 Juni, 713 Philippikos Bardanes
Juni 713 hadi 715 Anastasios II katibu wa Philippikos
715 hadi 717 Theodosius III

Nasaba ya Isauri hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
717 hadi 18 Juni, 741 Leo III
Juni 741 hadi 741 Konstantino V
741 hadi 743 Artabasdos waziri chini ya Leo III
743 hadi 14 Septemba, 775 Konstantin V awamu yake ya pili
Septemba 775 hadi 8 Septemba, 780 Kaisari Leo IVLeo IV mwana wa Konstantino V
Septemba 780 hadi 15 Agosti, 797 Konstantino VI mwana wa Leo IV
15 Agosti, 797 hadi 802 Malkia Irene mama ya Konstantino VI

Nasaba ya Nikephoros hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
802 hadi 26 Julai, 811 Nikeforo I
Julai 811 hadi Agosti 811 Staurakios mwana wa Nikeforo I
811 hadi Juni 813 Michael I Rangabe alimwoa binti wa Nikeforo I

Bila nasaba hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
Julai 813 hadi 25 Desemba, 820 Leo V

Nasaba ya Frigia hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
25 Desemba, 820 hadi Oktoba 829 Mikaeli II mke wake alikuwa binti Konstantino VI
Oktoba 829 hadi 20 Januari, 842 Theophilos mwana wa Mikaeli II, alikuwa Kaizari-Mshiriki tangu 820
20 Januari, 842 hadi Novemba 855 Malkia Theodora I mke wa Theophilos, alimtawalia mwana wake
Novemba 855 hadi 23 Septemba, 867 Mikaeli III mwana wa Theophilos, alitawala kumpitia mamake tangu 842

Nasaba ya Makedonia hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
23 Septemba, 867 hadi 29 Agosti, 886 Basili I alimwoa mjane wa Mikaeli III
29 Agosti, 886 hadi 11 Mei, 912 Leo VI mwana wa Basili I, Kaizari-Mshiriki tangu 870
11 Mei, 912 hadi 6 Juni, 913 Alexander III mwana wa Basili I, Kaizari-Mshiriki tangu 879
6 Juni, 913 hadi 9 Novemba, 959 Konstantino VII mwana wa Leo VI, Kaizari-Mshiriki tangu 911
919 hadi 944 Romano I baba mkwe wa Konstantino VII aliyemtawalia
959 hadi 15 Machi, 963 Romano II mwana wa Konstantino VII
3 Julai, 963 hadi Desemba 969 Nikeforo II alimwoa mjane wa Romano II
Desemba 969 hadi 10 Januari, 976 Yohane I alimwoa dada wa Konstantino VII
Januari 976 hadi 15 Desemba 1025 Basili II mwana wa Romano II
15 Desemba 1025 hadi 11 Novemba 1028 Konstantino VIII mwana wa Romano II, Kaizari-Mshiriki tangu 976
11 Novemba 1028 hadi 1050 Malkia Zoe binti Konstantino VIII
11 Novemba 1028 hadi 11 Aprili 1034 Romano III mume wa kwanza wa Zoe
Aprili 1034 hadi 10 Desemba 1041 Mikaeli IV mume wa pili wa Zoe
10 Desemba 1041 hadi Aprili 1042 Mikaeli V Mpwa wa Mikaeli IV
Aprili 1042 hadi Juni 1042 Malkia Theodora II Malkia-Mshiriki na dada yake, Zoe
Juni 1042 hadi 11 Januari 1055 Konstantino IX mume wa tatu wa Zoe
11 Januari 1055 hadi Agosti 1056 Malkia Theodora II awamu yake ya pili

Bila nasaba hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
21 Agosti 1056 hadi 31 Agosti 1057 Mikaeli VI jenerali aliyeteuliwa na Theodora II

Nasaba ya akina Komnenos hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
8 Juni 1057 hadi 25 Desemba 1059 Isaak I alijiuzulu kwa sababu ya ugonjwa

Nasaba ya akina Doukas hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
Desemba 1059 hadi 21 Mei 1067 Konstantino X aliteuliwa na Isaak I
21 Mei 1067 hadi 31 Machi 1078 Mikaeli VII mwana wa Konstantino X
Januari 1068 hadi 24 Oktoba 1071 Romano IV alimwoa mjane wa Konstatino X; Kaizari-Mshiriki na Michael VII
7 Januari 1078 hadi 4 Aprili 1081 Nikeforo III alimwoa mke wa Mikaeli VII wakati ndoa haijatengwa

Nasaba ya akina Komnenos hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
4 Aprili 1081 hadi 15 Agosti 1118 Alexios I Mpwa wa Isaak I
15 Agosti 1118 hadi 8 Aprili 1143 Yohane II mwana wa Alexios I
8 Aprili 1143 hadi 24 Septemba 1180 Manuel I mwana wa Yohane II
24 Septemba 1180 hadi Novemba 1183 Alexios II mwana wa Manuel I
Septemba 1183 hadi 12 Agosti 1185 Andronikos I mpwa wa Yohane II

Nasaba ya akina Angelos hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
12 Agosti 1185 hadi 8 Aprili 1195 Isaak II
8 Aprili 1195 hadi 1 Agosti 1203 Alexios III kaka wa Isaak II
1 Agosti 1203 hadi Januari 1204 Isaak II awamu yake ya pili; Kaizari-Mshiriki na mwana wake
1 Agosti 1203 hadi Januari 1204 Alexios IV mwana wa Isaak II
Januari 1204 hadi 12 Aprili 1204 Alexios V alimwoa binti Alexios III

Nasaba ya akina Laskaris hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
Aprili 1204 hadi 1205 Konstantino Laskaris hakuvishwa taji, kwa hiyo hahesabiwi kama Konstantino XI
1205 hadi Novemba 1222 Theodor I kaka wa Konstantino Laskaris
Novemba 1222 hadi 3 Novemba 1254 Yohane III mkwe mwana wa Theodor I
3 Novemba 1254 hadi Agosti 1258 Theodor II mwana wa Yohane III
Agosti 1258 hadi Agosti 1261 Yohane IV mwana wa Theodor II

Nasaba ya akina Palaiologos hariri

Miaka ya Utawala Jina la Kaizari Maelezo
1259 hadi 11 Desemba 1282 Mikaeli VIII
11 Desemba 1282 hadi Mei 1328 Andronikos II mwana wa Mikaeli VIII
Mei 1328 hadi 15 Juni 1341 Andronikos III mjukuu wa Andronikos II
15 Juni 1341 hadi Mei 1347 Yohane V mwana wa Andronikos III
Mei 1347 hadi 1354 Yohane VI baba mkwe wa Yohane V
1354 hadi 12 Agosti 1376 Yohane V awamu yake ya pili
12 Agosti 1376 hadi 1379 Andronikos IV mwana wa Yohane V
18 Oktoba 1377 hadi 1379 Yohane VII Kaizari-Mshiriki na Andronikos IV
1379 hadi 1390 Yohane V awamu yake ya tatu
miezi michache 1390 Yohane VII awamu yake ya pili
1390 hadi 16 Februari 1391 Yohane V awamu yake ya nne
16 Februari 1391 hadi 21 Julai 1425 Manuel II mwana wa John V; Kaizari-Mshiriki tangu 1373
1399 hadi 1402 Yohane VII awamu yake ya tatu; alimtawalia Manuel II
21 Julai 1325 hadi 31 Oktoba 1448 Yohane VIII mwana wa Manuel II
Januari 1449 hadi 29 Mei 1453 Konstantino XI mwana wa Manuel II