Orso wa Ravenna (alifariki Ravenna, Emilia-Romagna, Italia, 13 Aprili 425 hivi) alikuwa askofu wa mji huo wa Italia Kaskazini kwa miaka 26[1].

Mt. Orso katika mozaiki.

Alihamishia Ravenna kutoka Classe makao makuu ya jimbo akatabaruku kanisa kuu la Ufufuko sikukuu ya Pasaka, hatimaye alifariki katika sherehe hiyo miaka ya baadaye.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Aprili[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.