Papa Klementi VII

Papa wa Kanisa Katoliki kutoka 1523 hadi 1534

Papa Klementi VII (26 Mei 147825 Septemba 1534) alikuwa Papa kuanzia tarehe 19/26 Novemba 1523 hadi kifo chake[1]. Alitokea Firenze, Italia[2].

Papa Klementi VII.

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Giulio di Giuliano de' Medici.

Alishiriki katika vita kati ya Kaizari Karoli V wa Ujerumani-Hispania na Mfalme Fransisko I wa Ufaransa, akisimama kwanza na kaizari, baadaye na mfalme. Mwaka 1527 alikamatwa baada ya Roma kutekwa na jeshi la kaizari. Katika amani ya mwaka 1529, wakati wa mashambulio ya Waturuki dhidi ya Vienna, alirudishwa uhuru wake pamoja na utawala juu ya Dola la Papa katika Italia ya Kati, akikubali kipaumbele cha kaizari juu ya Italia ya Kaskazini. Mwaka 1530 alimwekwa Karolo V wakfu kama kaizari wa Dola Takatifu la Kiroma.

Katika miaka 1529 hadi 1534 Klementi VII aliwasiliana mara kwa mara na Mfalme Henry VIII wa Uingereza aliyetaka kibali cha Papa kutengana na mke wake wa kwanza. Papa alipokataa, mfalme aliagiza bunge lake kutangaza uhuru wa Kanisa la Uingereza; hatimaye Papa alimtenga mfalme Henry na Kanisa Katoliki kwenye mwaka 1534.

Alimfuata Papa Adrian VI akafuatwa na Papa Paulo III.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Klementi VII kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.