Paulo Chong Hasang

Paulo Chong Hasang (1794 au 1795Seoul, 22 Septemba 1839) alikuwa mmojawao Wafiadini wa Korea.[1]

Katekista huyo na wafiadini wenzake 102 walitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa watakatifu tarehe 6 Mei 1984.

Sikukuu ya Wafiadini wa Korea inaadhimishwan kila tarehe 20 Septemba, ila ya kwake mwenyewe ni siku ya kifodini chake, alipokatwa kichwa, baada ya kuongoza Wakatoliki wa nchi hiyo kwa miaka 20[2].

Maisha hariri

Mtoto wa mfiadini Augustino Jeong Yak-Jong na mjukuu wa mwanafalsafa Yohane Jeong Yak-Yong, ambao walikuwa kati ya Wakorea wa kwanza kuongokea dini ya Ukristo na kuandika katekisimu ya kwanza ya Kanisa Katoliki kwa Kikorea ("Jugyo Yoji").

Yakjong alipouawa pamoja na kaka wa Hasang, mke wake na watoto wengine waliachwa wakahamia vijijini. Hasang alikuwa na umri wa miaka saba.

Kisha kukua, Hasang aliajiriwa na afisa wa serikali, akapata hivyo nafasi ya kusafiri mara kadhaa hadi Beijing, alipomsihi askofu wa huko atume mapadri Korea, akamuandikia Papa Gregori XVI akimuomba aanzishe jimbo huko, jambo lililofanyika mwaka 1825.

Miaka michache baadaye, askofu Laurent-Marie-Joseph Imbert na mapadri wawili walitumwa huko. Askofu alitambua sifa za Hasang to akamfundisha Kilatini na teolojia, lakini alipotaka kumpa daraja takatifu ilizuka dhuluma dhidi ya Wakristo.

Hasang alikamatwa akampa hakimu tamko la maandishi la kutetea Ukatoliki. Kisha kulisoma, hakimu alimjibu, "Wewe uko sahihi katika yale uliyoyaandika; lakini mfalme amekataza dini hiyo, hivyo ni wajibu wako kuikataa." Hasang alijibu, "Nimekuambia mimi ni Mkristo, na nitakuwa hivyo hadi kifo changu."

Basi, Hasang aliteswa kwa namna mbalimbali bila kupotewa na utulivu wake. Hatimaye alisulubiwa akiwa na umri wa miaka 45.[3]

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.