Persepolis (kwa Kiajemi cha Kale: Pars<nowiki>'a; kwa Kifarsi: تخت جمشید, Takht-e Jamshid) ilikuwa mmoja kati ya miji mikuu minne katika Uajemi ya Kale wakati wa nasaba ya Waakhameni.

Jumba la Tachar, Persepoli
Filamu inayoonyesha jinsi Persepolis ilivyoonekana kabla ya kuharibika.

Waajemi wa kale waliiita Parsa, maana "Pars" ilikuwa moja ya majimbo makuu ya milki yao na Uajemi yenyewe. Kwa hiyo jina lilimaanisha "mji wa Waajemi". Persepolis (kwa Kigiriki: Περσες πόλις perses polis) ni tafsiri ya jina kwa Kigiriki. Katika Iran ya leo panaitwa "Takht-e-Jamshid" (Kiti cha Enzi cha Jamshid).

Hakuna uhakika kama ulikuwa mji kamili au zaidi tu jumba kubwa la kifalme. Ujenzi ulianza mnamo 515 KK chini ya mfalme Dario I. Wafalme waliomfuata waliendelea kuipanua. Lote liliharibika mnamo mwaka 330 KK wakati jeshi la Wagiriki chini ya Aleksander Mkuu walipovamia Uajemi.

Jengo kubwa huko Persepolis ni ukumbi wa Apadana wenye nguzo 72.

Persepolis imekubaliwa katika orodha ya Urithi wa Dunia wa UNESCO tangu mwaka 1979.

Viungo vya Nje hariri