Perth
Perth ni mji mkuu wa jimbo la Australia Magharibi uliopo kwenye kingo za Mto Swan.
Nchi | Australia |
Jimbo / Mkoa | Australia Magharibi |
Anwani ya kijiografia | 31°57′8″S 115°51′32″E / 31.95222°S 115.85889°E |
Kimo | mita |
Eneo | km2 6,417.9 |
Wakazi | 2,059,484 [1] |
Msongamano wa watu | 320.8969 / km2 |
Mahali | km 3288 kutoka Sydney |
Kuna wakazi karibu watu milioni 2.1 wanaoishi katika jiji hilo. [2] Ni mji mkubwa wa nne huko Australia, baada ya Sydney, Melbourne na Brisbane.
Perth ilianzishwa mnamo 1829 na nahodha James Stirling; huyu baharia alikuwa mwenyeji wa Uskoti hivyo alitumia jina la mji Perth wa Uskoti.
Perth ni maarufu kwa mchanga wake mweupe, mweupe. Fukwe zake ni bora kwa kuogelea. Kivutio maarufu cha watalii cha ndani ni Kisiwa cha Rottnest, ambacho kinakaliwa na wanyama wadogo wa kienyeji wanaoitwa Quokkas. Kivutio kingine maarufu ni Kings Park, ambayo ni mojawapo ya mbuga kubwa za jiji ulimwenguni.
Vyuo vikuu hariri
Perth ina vyuo vikuu vifutavyo: [3]
- Chuo Kikuu cha Australia Magharibi
- Chuo Kikuu cha Murdoch
- Chuo Kikuu cha Curtin
- Chuo Kikuu cha Edith Cowan
- Chuo Kikuu cha Notre Dame (Australia Magharibi) (kibinafsi)
Tabianchi hariri
Tabianchi ni nusutropiki, kuna kipindi cha joto ambako hasa Januari na Februari hufikia viwango vya zaidi ya °C 31. Kinyume chake kuna miezi inayofanana na eneo la Mediteranea, katika miezi ya Juni hadi Agosti jotoridi hushuka chini °C 20 na kiasi cha mvua kinazidi milimita 120; jalidi (chini ya °C 0) hutokea mara chache. [4] [5] [6]
Marejeo hariri
- ↑ "3218.0 – Regional Population Growth, Australia, 2017–18". Australian Bureau of Statistics. 27 March 2019. Iliwekwa mnamo 22 April 2019. Check date values in:
|date=, |accessdate=
(help) ERP at 30 June 2018. - ↑ "Regional Population Growth, Australia 2008–2009". Australian Bureau of Statistics. 30 March 2010. Check date values in:
|date=
(help) - ↑ Western Australian Universities Archived 5 Septemba 2012 at the Wayback Machine. (accessed 2007-02-27)
- ↑ "Perth is Australia's windiest city | Did You Know That..?". didyouknowthat.org. 2011 [last update]. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-06. Iliwekwa mnamo August 31, 2011. Check date values in:
|date=, |accessdate=
(help) - ↑ "The Great Australian Weather Debate". gungahlinweather.com. 2008 [last update]. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-01. Iliwekwa mnamo August 31, 2011.
officially be call
Check date values in:|date=, |accessdate=
(help) - ↑ "Did you know that...about Australia?". upfromaustralia.com. 2011 [last update]. Iliwekwa mnamo August 31, 2011. Check date values in:
|date=, |accessdate=
(help)
Makala hii kuhusu maeneo ya Australia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Perth kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |