Petro Juliani Eymard

Petro Juliani Eymard (La Mure, Grenoble, Ufaransa, 4 Februari 1811 – La Mure, 1 Agosti 1868) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki.

Picha ya mtakatifu Petro Juliani Eymard.

Kwanza mwanajimbo, baadaye alijiunga na Shirika la Maria na kutokana na imani yake kubwa kwa fumbo la ekaristi alianzisha mashirika mawili ya kitawa, moja la kiume na lingine la kike ili kuhamasisha na kueneza ibada kwa sakramenti hiyo kuu[1].

Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI tarehe 12 Julai 1925, halafu mtakatifu na Papa Yohane XXIII tarehe 9 Desemba 1962. Papa Yohane Paulo II alimtangaza Eymard "Mtume wa Ekaristi".[2]

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 2 Agosti[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.