Poloni (kutoka kilatini Polonia kwa nchi ya Poland) ni nusumetali au metaloidi nururifu yenye namba atomia 84 katika mfumo radidia. Uzani atomia ni 209.

Poloni (Polonium)
Jina la Elementi Poloni (Polonium)
Alama Po
Namba atomia 84
Mfululizo safu Simetali
Uzani atomia 209
Valensi 2, 8, 18, 32, 18, 6
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 527 K (254  °C)
Kiwango cha kuchemka 1235 K (962 °C)
Hali maada mango
Mengineyo Poloni ni nururifu; nusumaisha ya isotopi zake ni kati ya mikrosekondi hadi miaka 103

Poloni ni elementi nururifu sana na hatari kwa afya. Isotopi inayopatikana zaidi ni 210Po yenye nusumaisha ya siku 138 inayobungua kuwa metali ya risasi.

Kutokana na nusumaisha fupi ni elementi haba. Kiasili hupatikana kwa viwango vidogo sana katika mitapo ya Urani inapotokea kutokana na mbunguo wa radi na radoni. Siku hizi takriban gramu 100 zatengenezwa kila mwaka kwa kutupia neutroni kwa bismuti katika maabara hasa Urusi.

Poloni ilitambuliwa pamoja na Radi mara ya kwanza 1898 na mwanakemia Mpoland Marie Curie na mume wake Mfaransa Pierre.

Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Poloni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Poloni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.