Ponsyano wa Spoleto

Ponsyano wa Spoleto (kwa Kilatini: Pontianus; 156 - Spoleto, Umbria, Italia, 14 Januari, 175) alikuwa kijana Mkristo aliyefia dini yake hiyo kwa kupigwa kikatili na hatimaye kuchomwa kwa upanga wakati wa dhuluma ya kaisari Antoninus Pius au Marcus Aurelius[1][2].

Mt. Pontianus, mchoro wa Spinello Aretino, 1383 hivi ulioko Hermitage Museum, St.Petersburg, Russia.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Januari[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Festa di S. Ponziano, patrono di Spoleto (it). Archidiocesi di Spoleto-Norcia (14 January 2013).
  2. Santi e Beati della Diocesi (it). Archidiocesi di Spoleto-Norcia.
  3. Martyrologium Romanum
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.