Puerto Rico ni nchi katika Bahari ya Karibi ambayo ni eneo la kushirikishwa la Marekani katika visiwa vya Antili Kubwa.

Puerto Rico
Ramani ya Puerto Rico

Iko upande wa mashariki wa Jamhuri ya Dominika na upande wa magharibi ya Visiwa vya Virgin.

Funguvisiwa la Puerto Rico linajumuisha kisiwa kikuu cha Puerto Rico pamoja na visiwa vidogo kama vile Mona, Vieques, Monito, Desecheo, Caja de Muertos, Pajaros, Icacos, Palominos, Palominitos, Culebrita, na Culebra.

Jina la Puerto Rico kwa Kihispania humaanisha "bandari tajiri".

Historia hariri

Ilikuwa koloni la Hispania mpaka ilipovamiwa na Marekani tarehe 25 Julai 1898, wakati wa Vita ya Marekani dhidi Hispania na kutawaliwa kama koloni hadi mwaka 1917 ambapo watu wa Puerto Rico walipewa uraia wa Marekani na kiwango cha utawala katika mambo ya ndani.

Tangu mwaka 1948 gavana amechaguliwa na wananchi, si kuteuliwa tena na rais wa Marekani.

Puerto Rico si jimbo kamili la Marekani bali nchi inayojitawala katika mambo ya ndani ilhali siasa ya nje na mambo ya uchumi hutawaliwa na Marekani.

Wakazi ni raia wa Marekani lakini hawashiriki katika uchaguzi wa rais. Kuna mwakilishi wa Puerto Rico katika bunge la Washington lakini hapigi kura.

Watu wa Puerto Rico humchagua Gavana na wabunge wao.

Katika kura za miaka 1967 na 1993 walikataa kulenga uhuru lakini walikataa pia kuwa jimbo kamili la Marekani, wakapendelea hali ya eneo la kushirikishwa. Kumbe mwaka 2012, kura zilionyesha kuwa 54% wanapenda badiliko, hasa kujiunga na Marekani kama jimbo la 51.

Watu hariri

Tangu mwaka 2000 idadi ya wakazi inazidi kupungua na kuzeeka.

Karibu nusu ya wakazi wote wanajitambulisha kwa machotara, halafu kama Wazungu (17.1%) na Waafrika (7%) kwa asili. Vipimo vinaonyesha kuwa Wazungu wamechangia 64% na Waafrika 25%, wakati Waindio wamechangia 11% ya DNA ya wakazi wa sasa.

Lugha rasmi ni kwanza Kihispania (inayozungumzwa kawaida na 95% za wananchi), halafu Kiingereza.

Upande wa dini, walio wengi ni Wakristo, hasa Wakatoliki (56%) na Waprotestanti (33%).

  Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Puerto Rico kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Puerto Rico kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.