Dana Elaine Owens (amezaliwa tar. 18 Machi 1970),[1] anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Queen Latifah, ni rapa, mwigizaji, na mwimbaji kutoka nchini Marekani. Kazi zake Queen Latifah katika muziki, filamu na televisheni zimepelekea kupata tuzo ya Golden Globe, Screen Actors Guild Awards mbili, Image Awards mbili, Grammy Award, amechaguliwa mara sita kwenye Grammy, na kuchaguliwa tena kwenye Emmy Award na Academy Award.

Queen Latifah

Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Dana Elaine Owens
Pia anajulikana kama Queen Latifah, The Queen of Rap
Amezaliwa 18 Machi 1970 (1970-03-18) (umri 54)
Asili yake Newark, New Jersey, Marekani
Aina ya muziki R&B, soul, jazz, hip hop
Kazi yake Mwimbaji-mtunzi, mtayarishaji wa rekodi, rapa, mwigizaji, mwongeaji, mtunzi wa vitabu
Ala Piano, sauti
Miaka ya kazi 1988–mpaka sasa
Studio Verve, Interscope, Motown, Tommy Boy, Warner Bros., PolyGram
Tovuti www.QueenLatifah.com

Maisha ya awali hariri

Latifah alizaliwa na kukulia mjini Newark, New Jersey, binti wa Rita, mwalimu wa shule ambaye alifanya kazi katika shule ya Irvington High School ya mjini New Jersey, na Lancelot Owens, Sr, ambaye ni afisa wa polisi.[2][3][4] Wazazi wake walitalikiana wakati Latifah akiwa na umri wa miaka kumi. Latifah alikulia katika kanisa la Kibaptist.[5] Jina lake la kisanii, Latifah (لطيفة), maana yake "laini" na "mwanana" kwa Kiarabu, alipewa jina hilo na binamu yake wakati ana umri wa miaka minane. Daima msichana shupavu, urefu wa futi 5'10" wa Latifah alikuwa mtu wa mbele katika timu ya mpira wa kikapu ya shuleni kwake.[6][7] Aliimba kipengele cha "Home" kutoka katika filamu ya muziki ya The Wiz katika mchezo wa kuigiza wa shuleni kwake.[8]

Kazi za muziki hariri

Mwanzo (1988–1989) hariri

Latifah alianza beatboxing kwa ajili kundi la rap la Ladies Fresh. Latifah alikuwa mmoja kati ya wanachama wa toleo halisi la Flavor Unit, ambalo, kwa kipindi hicho, -likuwa kundi la Ma-MC walioungana na mtayarishaji DJ Mark the 45 King. Mnamo 1988, DJ Mark the 45 King alisikia toleo la mfano (demo) la single ya Latifah "Princess of the Posse" na kutoa demo ile kwa Fab Five Freddy, ambaye alikuwa mtangazaji wa Yo! MTV Raps.

Kurap (1989–2002) hariri

Freddy alimsaidia Latifah kuingia mkataba na Tommy Boy Records, ambao ndiyo waliotoa albamu ya kwanza ya Latifah, All Hail the Queen mnamo 1989, akiwa na umri wa miaka kumi na tisa. Mwaka huo, alionekana kama mwamuzi kwenye UK label Music of Life album "1989—The Hustlers Convention (live)". Mnamo 1998, ashirikiana na Ro Smith sasa ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Def Ro Inc. akaweza kutayarisha na kutoa albamu yake ya nne ya hip-hop, Order in the Court.

Kuimba (2003–2007) hariri

Baada ya Order in the Court, Latifah akahamia jumla katika uimbaji wa mashairi ya muziki wenye viwango vya soul na jazz, ambapo awalia alikuwa akifanya kama ziada wakati anafanya rekodi za hip hop hapo awali. Mnamo 2004, ametoa albamu ya soul/jazz The Dana Owens Album. Mnamo tar. 11 Julai 2007, Latifah aliimba katika Hollywood Bowl mjini Los Angeles ikiwa kama kifunguzi cha tamasha la moja kwa moja la jazz. Kabla ya kundi la watu wanaizidi kiaisi cha 12,400, nyuma yake kulikuwa na watu wanaopig vyombo wakiwa kumi na wengine watatu waimbaji-wa-kwa-nyuma, huitwa The Queen Latifah Orchestra. Baadaye 2007, Latifah ametoa albamu iliyoitwa Trav'lin' Light. Jill Scott, Erykah Badu, Joe Sample, George Duke, Christian McBride, na Stevie Wonder wameuza sura ndani yake.[9] It was nominated for a Grammy in the "Best Traditional Pop Vocal Album" category.[10]

Mnamo 2009, Latifah, akiwa pamoja na Jubilation Choir, wamerekodi kibao kwenye albamu ya Oh Happy Day: An All-Star Music Celebration, wameurudia wimbo wa Oh Happy Day wa kina Edwin Hawkins Singers waliopatia umaarufu mnamo 1969.[11]

Kurudi katika hip hop (2008–mpaka sasa) hariri

Mnamo 2008, Latifah aliulizwa kama anaweza kutengeneza albamu nyingine ya hip hop. Alinukuliwa akisema kwamba albamu isha-kamilika tayari na itaitwa "All Hail the Queen II". Kulikuwa na fununu ya kwamba albamu ingeitwa "The 'L' Word". Alipoulizwa kuhusu fununu hizo, alieleza kwamba lilikuwa jaribio lake tu la "kuvuruga mibichwa ya watu" wanamzania kwamba ni msagaji.[12] Mnamo tar. 12 Septemba 2008, Rolling Stone waliitoa taarifa ya kwamba Queen Latifah anapika albamu yake mpya itakayoitwa Persona. Kasha la albamu hii linafanana na mchezo wa videoo wa Shin Megami Tensei: Persona. Wimbo "Cue the Rain" ulitolewa ukiwa kama single kiongozi kutoka katika albamu. Pia kuna wimbo kaimba na Missy Elliott.[13]

Filamu na televisheni hariri

Kazi za awali (1993–2001) hariri

Kuanzia 1993-1998, Latifah alikuwa na uhusika katika ucheshi wa Living Single uliokuwa ukirushwa na Fox, pia alitunga na kuimba kwenye kibwagizo cha ucheshi huo. Alianza kazi zake za uigizaji wa filamu kwenye uhusika-saidizi wa mnamo 1991 na 1992 kwenye filamu za House Party 2, Juice, na Jungle Fever. Alikuwa na kipindi chake mwenyewe cha majadiliano kilichokwenda kwa jina la The Queen Latifah Show, kuanzia mwaka wa 1999 mpaka 2001. Pia alipata kuwa na uhusika wa kurudia-rudia kwenye msimu wa pili (1991-1992) wa kipindi mashuhuri cha NBC, The Fresh Prince of Bel-Air. Amepata kucheza kama mgeni mwalikwa kwenye ucheshi wa Hangin' with Mr. Cooper mnamo 1993. Latifah ameonekana katika filamu kali ya mwaka wa 1996, Set It Off na kisha baadaye kupata uhusika-saidizi katika filamu ya Holly Hunter , Living Out Loud (1998).[4] Amecheza kama Thelma mnamo 1999 kwenye filamu ya Jeffrey Deavers, The Bone Collector, akiwa sambamba na Denzel Washington na Angelina Jolie.

Mafanikio (2002–mpaka sasa) hariri

Vitabu hariri

Latifah alitunga kitabu kuhusu maisha yake, ambacho kilichapishwa mnamo 1999 na HarperCollins - Ladies First: Revelations of a Strong Woman (ISBN 0-688-15623-1).

Maisha binafsi hariri

Diskografia hariri

Studio albums hariri

Makompilesheni hariri

Filmografia hariri

Mwaka Filamu Uhusika Maelezo
1991 Jungle Fever Lashawn
House Party 2 Zora
1992 Juice Ruffhouse M.C.
1996 Set It Off Cleopatra 'Cleo' Sims American Black Film Festival Award for Best Actress
Nominated — Independent Spirit Award for Best Supporting Female
Nominated — NAACP Image Award for Outstanding Actress in a Motion Picture
1997 Hoodlum Sulie
1998 Living Out Loud Liz Bailey Nominated — NAACP Image Award for Outstanding Supporting Actress in a Motion Picture
Sphere Alice "Teeny" Fletcher
1999 The Bone Collector Thelma Nominated — Black Reel Award for Theatrical - Best Supporting Actress
Nominated — NAACP Image Award for Outstanding Supporting Actress in a Motion Picture
2002 Chicago Matron "Mama" Morton Black Reel Award for Theatrical - Best Supporting Actress
Broadcast Film Critics Association Award for Best Cast
Screen Actors Guild Award for Outstanding Performance by a Cast in a Motion Picture
Nominated — Academy Award for Best Supporting Actress
Nominated — BAFTA Award for Best Actress in a Supporting Role
Nominated — Golden Globe Award for Best Supporting Actress – Motion Picture
Nominated — Phoenix Film Critics Society Award for Best Cast
Nominated — Screen Actors Guild Award for Outstanding Performance by a Female Actor in a Supporting Role
Roberto Benigni's Pinocchio Dove (English voice)
Brown Sugar Francine
Nominated — NAACP Image Award for Outstanding Actress in a Motion Picture
2003 Scary Movie 3 Aunt Shaneequa
Bringing Down the House Charlene Morton Producer
NAACP Image Award for Outstanding Actress in a Motion Picture
Nominated — BET Comedy Award for Outstanding Lead Actress in a Box Office Movie
Nominated — Black Reel Award for Film - Best Actress
Nominated — Nickelodeon Kids' Choice Award for Favorite Movie Actress
2004 Taxi Belle
The Cookout Security Guard (also producer)
Barbershop 2: Back in Business Gina BET Comedy Award for Outstanding Supporting Actress in a Box Office Movie
2005 Beauty Shop Gina Norris Producer
Nominated — BET Comedy Award for Outstanding Lead Actress in a Theatrical Film
Nominated — Black Movie Award for Outstanding Performance by an Actress in a Leading Role
Nominated — Black Reel Award for Film - Best Actress
Nominated — NAACP Image Award for Outstanding Actress in a Motion Picture
2006 Stranger Than Fiction Penny Escher
Ice Age The Meltdown Ellie Voice
Nickelodeon Kids' Choice Award for Favorite Voice from an Animated Movie
Last Holiday Georgia Byrd Nominated — Black Movie Award for Outstanding Performance by an Actress in a Leading Role
Nominated — NAACP Image Award for Outstanding Actress in a Motion Picture
2007 Life Support Ana Producer
Golden Globe Award for Best Actress – Miniseries or Television Film
Gracie Allen Award for Outstanding Female Lead - Drama Series or Special
NAACP Image Award for Outstanding Actress in a Television Movie, Mini-Series or Dramatic Special
Screen Actors Guild Award for Outstanding Performance by a Female Actor in a Miniseries or Television Movie
Nominated — Primetime Emmy Award for Outstanding Lead Actress – Miniseries or a Movie
Nominated — Prism Award for Performance in a TV Movie or Miniseries
Nominated — Satellite Award for Best Actress – Miniseries or Television Film
Hairspray Motormouth Maybelle Hollywood Film Festival Award for Best Ensemble Cast
Nominated — Broadcast Film Critics Association Award for Best Song
Nominated — NAACP Image Award for Outstanding Supporting Actress in a Motion Picture
Nominated — Screen Actors Guild Award for Outstanding Performance by a Cast in a Motion Picture
Arctic Tale Mwadithiaji
The Perfect Holiday Mrs. Christmas Mtayarishaji
2008 Mad Money Nina Brewster
What Happens in Vegas... Dr. Twitchell
The Secret Life of Bees August Boatwright Black Reel Award for Best Actress
Hollywood Film Festival Award for Best Ensemble Cast
Nominated — Black Reel Award for Best Ensemble
Nominated — NAACP Image Award for Outstanding Actress in a Motion Picture
2009 Ice Age: Dawn of the Dinosaurs Ellie Sauti
2010 Valentine's Day Paula Thomas
Just Wright Leslie Wright Mtayarishaji
Hairspray 2: White Lipstick Motormouth Maybelle

Marejeo hariri

  1. Jason Buchanan, Allmovie (2008). "Queen Latifah:Biography". MSN. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-16. Iliwekwa mnamo 2008-09-04.  Unknown parameter |= ignored (help)
  2. Hyman, Vicki. "The Queen holds court", The Star-Ledger, 2007-07-18. Retrieved on 2007-07-21. Archived from the original on 2007-09-29. 
  3. Queen Latifah Biography (1970-)
  4. 4.0 4.1 Stated in interview on Inside the Actors Studio, 2006
  5. Queen Latifah Discusses God, Jesus, Rap, and Her New Movie, 'Last Holiday,' in this Beliefnet Interview - Beliefnet.com
  6. People.com bio
  7. "'Queen' Of Many Hats, Queen Latifah Makes Jump From Hip Hop Artist To Actress - CBS News". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-01-05. Iliwekwa mnamo 2010-03-04. 
  8. Queen Latifah | Music Artist | Videos, News, Photos & Ringtones | MTV
  9. "LATIFAH OPENING FATBURGER IN MIAMI: Plus, new album due September 25.". EURweb. 17 Julai 2007. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-08-20. Iliwekwa mnamo 2010-03-04. 
  10. "GRAMMY.com". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-12-08. Iliwekwa mnamo 2010-03-04. 
  11. "Jon Bon Jovi, Queen Latifah go gospel for "Day"". Reuters. 27 Machi 2009. 
  12. "Lesbian album scares Queen Latifah”". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-08-13. Iliwekwa mnamo 2010-03-04. 
  13. "Queen Latifah Returns to Hip-Hop With Dre on LP She Nearly Named “The L Word”". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-08-30. Iliwekwa mnamo 2010-03-04.  Unknown parameter |= ignored (help)

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: