Rais wa Ujerumani ni mkuu wa dola katika Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani.

Bendera ya Rais wa Ujerumani

Kazi yake ni kuwa alama ya umoja wa taifa, lakini katika mfumo wa serikali ya kibunge nchini Ujerumani hana madaraka mengi. Madaraka muhimu ya kisiasa ni kama yafuatayo

  • rais anapaswa kutia sahihi kwa kila sheria iliyopitishwa bungeni. Hapa anaweza kukataa akiona sababu muhimu ya kwamba sheria hailingani na katiba. Akikataa bunge ina njia ya kusahihisha sheria au kumshtaki ais mbele ya mahakama kuu. Tangu 1949 maraisi wa Ujerumani walikataa mara 9 kutia sahihi wakalazimisha serikali na bunge kubadilisha sheria.
  • rais anaamua kama bunge inavunjwa baada ya chansella kushindwa katika swali la imani katika serikali; chansella kama kiongozi wa serikali anaweza kudai kura ya bunge kama ina imani katika serikali. Kama swali hili linakataliwa na wabunge wengi chansella anaweza kumwomba rais kuvunja bunge na uchaguzi wa bunge jipya. Lakini azimio liko mkononi mwa rais anayeweza kumteua kiongozi wingine kuunda serikali mpya.

Rais huchaguliwa kila baada ya miaka 5 na mkutano wa shirikisho (Bundesversammlung) ambao ni wabunge wote pamoja na idadi sawa ya wawakilishi wa mabunge ya majimbo.

Mshahara wa rais ni asilimia 90 za mshahara wa chansella wa Ujerumani. Katika mwaka 2010 hii ililingana na Euro 199,000; pamoja na hayo anapata Euro 78.000 marupurupu ya kando na kwa pesa hii analipa mishahara ya watumishi wa nyumba yake anayopata bure.

Orodha ya marais wa Ujerumani hariri

Marais wa Jamhuri ya Weimar (Reichspräsident) (1919-1933) hariri

# Picha Jina
(miaka ya maisha)
Tarehe ya kuanza Tarehe ya kwisha Chama
1   Friedrich Ebert
(1871-1925)
11 Februari 1919 28 Februari 1925 SPD
2   Paul von Hindenburg
(1847-1934)
12 Mei 1925 2 Agosti 1934 -
  Adolf Hitler
(1889-1945)
2 Agosti 1934 30 Aprili 1945 NSDAP
3   Karl Dönitz
(1891-1980)
30 Aprili 1945 23 Mei 1945 -

Marais wa Ujerumani ya Magharibi (1949–1990) hariri

Marais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani (Bundespräsident) hariri

# Picha Jina
(miaka ya maisha)
Tarehe ya kuanza Tarehe ya kwisha Chama
1   Theodor Heuss
(1884-1963)
13 Septemba 1949 12 Septemba 1959 FDP
2   Heinrich Lübke
(1894-1972)
13 Septemba 1959 30 Juni 1969 CDU
3   Gustav Heinemann
(1899-1976)
1 Julai 1969 30 Juni 1974 SPD
4   Walter Scheel
(born 1919)
1 Julai 1974 30 Juni 1979 FDP
5   Karl Carstens
(1914-1992)
1 Julai 1979 30 Juni 1984 CDU
6   Richard von Weizsäcker
(born 1920)
1 Julai 1984 30 Juni 1994 CDU

Marais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kijerumani (Präsident der Volkskammer) hariri

# Picha Jina
(miaka ya maisha)
Tarehe ya kuanza Tarehe ya kwisha Chama
  Wilhelm Pieck
(1876-1960)
11 Oktoba 1949 7 Septemba 1960 SED
1   Walter Ulbricht
(1893-1973)
12 Septemba 1960 1 Agosti 1973 SED
2   Willi Stoph
(1914-1999)
3 Oktoba 1973 29 Oktoba 1976 SED
3   Erich Honecker
(1912-1994)
29 Oktoba 1976 18 Oktoba 1989 SED
4   Egon Krenz
(1937-)
18 Oktoba 1989 6 Desemba 1989 SED
5   Manfred Gerlach
(1928-)
6 Desemba 1989 5 Aprili 1990 LDPD
  Sabine Bergmann-Pohl
(1946-)
5 Aprili 1990 2 Oktoba 1990 CDU

Marais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani (Bundespräsident) (1990-sasa) hariri

# Picha Jina
(miaka ya maisha)
Tarehe ya kuanza Tarehe ya kwisha Chama
6   Richard von Weizsäcker
(1920-)
since
1 Julai 1984
30 Juni 1994 CDU
7   Roman Herzog
(1934-)
1 Julai 1994 30 Juni 1999 CDU
8   Johannes Rau
(1931-2006)
1 Julai 1999 30 Juni 2004 SPD
9   Horst Köhler
(1943-)
1 Julai 2004 31 Mei 2010 CDU
10   Christian Wulff
(1959-)
2 Julai 2010 17 Februari 2012 CDU
11   Joachim Gauck
(1940-)
18 Machi 2012 sasa

Tazama pia hariri