Yucatan (tamka yu-ka-tan) ni rasi kubwa huko Amerika Kaskazini (au Amerika ya Kati, inategemea kama unaiona pekee na kaskazini). Rasi hii inatenganisha Bahari ya Karibi na Ghuba ya Mexico.

Peninsula ya Yucatán kama inavyoonekana kutoka anga-nje
Ramani inayoonyesha milima na lugha za Kimaya

Sehemu ya kaskazini ya rasi hiyo iko ndani ya Meksiko, ikigawiwa katika majimbo yake ya Yucatan, Campeche na Quintana Roo. Kusini ya rasi iko katika Guatemala na Belize. Upande wa mashariki kipo kisiwa kikubwa zaidi cha Meksiko ambacho ni Cozumel.

Kasoko ya Chicxulub iko kwenye pwani ya kaskazini. Ilisabishwa na pigo la asteroidi miaka milioni 65 iliyopita iliyoleta maafa makubwa duniani pamoja na kuangamizwa kwa dinosauri.

Historia hariri

Kabla ya kufika kwa Wahispania, Yucatan ilikuwa eneo la ustaarabu wa Wamaya. Walikuwa na miji mingi kama Chichen Itza, Tulum und Uxmal, na milki ndogo mbalimbali. Wahispania walivamia eneo kuanzia mwaka 1527 hadi 1547 ikawa sehemu ya Hispania Mpya. Kulikuwa na sehemu ndogo ambako utawala wa Wamaya uliendelea kwa siri.

Katika karne ya 19, baada ya kuporomoka kwa ukoloni wa Hispania, nchi za Amerika ya Kati zilipata uhuru na eneo la Yucatan liligombaniwa kati ya Meksiko na Gutemala. Mwaka 1841 Yucatan ilitangaza uhuru wake ikitawaliwa na Wakreoli (wakazi wenye asili ya Hispania) bila kushirikisha Wamaya. Wamaya wazalendo walitumia nafasi ya kuanzisha vita ya kupigania uhuru wao katika vita ndefu kuanzia mwaka 1847 hadi 1901. Mafanikio ya Wamaya yalisababisha Jamhuri ya Yucatan kurudi Meksiko, na hatimaye jeshi la Meksiko lilifaulu kugandamiza upinzani wa Wamaya.

Kwa miaka mingi sehemu za Yukatan zilikuwa chini ya mamlaka ya kijeshi hadi maeneo yake yalipewa hadhi ya kuwa majimbo kamili ya kujitawala ndani ya Meksiko.

  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.