Ratili (pia: ratli - kutoka Kiarabu رطل, ratl) ni kipimo cha kihistoria cha masi cha takriban nusu kilogramu au gramu 400-500.

Ni kati ya vipimo asilia vya Kiswahili, si kipimo sanifu cha kisasa.

Inalingana takriban na "pauni" (pound) ya Ulaya.

Ratili ilipokewa kutoka vipimo vya Kiarabu: "ratl" iliyotumiwa kwa jina hili katika sehemu nyingi za nchi za Kiislamu. Lakini uzani wa ratl ulikuwa tofauti kati ya nchi, majimbo na miji, kuanzia gramu 340 hadi zaidi ya kilogramu 2. Ratili ya Uswahilini ililingana zaidi na ratl jinsi ilivyotumiwa Uarabuni katika eneo la Makka iliyokuwa kidogo juu ya gramu 400.[1]

Ratili kama kipimo cha kihandisi na biashara hariri

Hadi leo "ratili" inatumiwa pale ambako matini za kiingereza zinatafsiriwa zinazotumia "[[:en:pound|]".

  • pau za reli zinatofautishwa mara nyingi kwa kutaja uzito kwa urefu na katika mfumo wa vipimo vya Uingereza ni "pound per yard" na kwa Kiswahili "ratili"[2]. Hapo ratili inalingana na pound ya Kiingereza ambayo ni gramu 453.59237.

Tanbihi hariri

  1. Makala "Makayil" katika The Encyclopedia of Islam, Leiden 1991, Vol VI, MAHK—MID
  2. linganisha taarifa kwenye tovuti ya TRL Archived 8 Septemba 2018 at the Wayback Machine. "kazi ya kutandika reli nzito ratili 80 imekamilika", habari ya 25 Machi 2017, iliangaliwa Aprili 2017

Marejeo hariri