Reni (kutoka jina la Kilatini "Rhenus" la mto Rhine) ni metali nzito na haba sana. Kikemia ni elementi ya mpito yenye kifupi cha Re na namba atomia 75 katika mfumo radidia.

Reni (Rhenium)
Reni katika testitubu
Reni katika testitubu
Jina la Elementi Reni (Rhenium)
Alama Re
Namba atomia 75
Mfululizo safu Metali ya mpito
Uzani atomia 98
Valensi 2, 8, 18, 32, 13, 2
Densiti 21.02
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 3459 K (3186 °C)
Kiwango cha kuchemka 5869 K (5596 °C)
Asilimia za ganda la dunia 1 · 10-7 %
Hali maada mango
Mengineyo

Tabia hariri

Reni ni metali ngumu na nzito. Hutokea katika mitapo ya molibdeni. Baada ya kuisafisha rangi yake ni kifedha-nyeupe. Kati ya elementi zote zisizo nururifu ni elementi haba sana.

Matumizi hariri

Kutokana na uhaba hakuna matumizi mengi. Inachanganywa hasa ndani ya aloi mbalimbali hasa na nikeli inapoongeza uimara kwa mfano ndani ya injini za ndege.


  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Reni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.