Kwa elementi na metali angalia Risasi (metali)

Risasi za bunduki na bastola

Risasi ni gimba dogo la metali linalorushwa kutoka kasiba ya bunduki. Mara nyingi risasi hutengenezwa kwa plumbi yaani metali inayoitwa pia "risasi". Jina la metali imekuwa jina kwa ajili ya silaha.

Risasi katika historia hariri

Zamani risasi zilitengenezwa kwa kwa kutumia plumbi pekee. Bunduki za zamani kama gobori ziliweza kurusha hata vipande vya mawe au vipande vidogo vya metali yoyote. Risasi ilipendezwa kutokana na uzito wake ulioipeleka mbali zaidi na kwa nguvu zaidi; pia ni metali inayoyeyushwa kirahisi kwa kutumia joto kidogo kuliko metali nyingine.

Hivyo askari mwenye gobori alitengeneza risasi kwa ajili ya bunduki yake kabla ya kila mapigano. Kwa kazi hii askari alikuwa na kifaa alimomwaga risasi iliyoyeyuka ikatoka kwa umbo la tufe. Alibeba baruti yake katika chupa, kumwaga kiasi cha baruti katika silaha, kuongeza risasi juu yake na kukandamiza yote kwa fimbo ndefu ndani ya kasiba ya silaha, halafu kuipashia moto kupitia shimo ndogo kando la kasiba.

Baadaye risasi zilifungwa katika karatasi pamoja na kiasi cha baruti kwa kila matumizi ya silaha. Hii ilikuwa ramia ya kwanza na askari alipaswa kufungua ramia kwa meno yake, kumwaga baruti katika bunduki na kuongeza risasi juu yake.

Katika karne ya 19 muundo wa bunduki imebadilika na kasiba imepata mifuo ndano yake kwa mwendo wa sukurubu iliipa risasi mwendo wa kuzunguka na kuongeza ukamilifu wa kupiga shabaha. Sasa ramia zilizotengenezwa kiwandani zilikuwa za metali hasa shaba na risasi ilibanwa kwenye kichwa cha ramia. Baruti iliwaka kwa pigo la sindano ya silaha na risasi ilirushwa nje.

Risasi za kisasa hariri

 
Ramia ya kisasa ina risasi inayorushwa pamoja na ganda lilaoshika baruti ndani yake

Siku hizi risasi zote zinatengenezwa kiwandani na kuuzwa kama sehemu ya ramia. Risasi yenyewe mara nyingi bado ni ya plumbi (elementi ya risasi) lakini kwa kawaida risasi ina koti ya metali gumu zaidi kama shaba au feleji.

Aina ya ganda inasababisha tabia tofauti tofauti za risasi. Ganda kamili ya kufunika risasi yote inaongeza nguvu; kama mtu anapigwa nayo risasi itapita kwenye mwili. Aina hii ni risasi ya kijeshi. Risasi kwa uwindaji zina ganda la sehemu tu inayopasuka wakati wa kupiga shabaha. Inaacha nichati yake katika shabaha maana yake ina nguvu zaidi ya kuua. Kufuatana na kanuni za kimatifa aina hii hairuhusiwi kwa matumizi ya kijeshi.

Kuna pia risasi zinazojaa metali nzito zaidi kuliko plumbi kama vile urani. Hizi zatumiwa kwa ajili ya shabaha gumu.

  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Risasi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.