Félix Rubén García Sarmiento (jina la kisanii: Rubén Darío; 18 Januari 18676 Februari 1916) alikuwa mshairi na mwandishi kutoka nchini Nikaragua. Maisha yake aliyatumia kama mwanahabari na balozi wa nchi yake.

Rubén Darío

Maisha hariri

Rubén Darío alizaliwa katika familia ya wastani akaanza kutunga mashairi tangu umri wa miaka 6. Tangu 1890 alifanya kazi ya mwandishi wa habari kwa magazeti ya Nikaragua akatumwa kuwa mwandishi mkazi katika nchi mbalimbali kama Chile, Argentina, Marekani hadi Ulaya.

Miaka 1908-1910 alikuwa balozi wa Nikaragua nchini Hispania lakini alipaswa kuacha kazi baada ya badiliko la serikali ya nyumbani.

Aliaga dunia nchini Nikaragua mwaka 1916.

Alipata umaarufu kwa mashairi yake ya "Prosas Profanas" (1896; mashairi ya kawaida).

  Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rubén Darío kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.