Saba Kijana (Collesano, Sicilia, 910 hivi - Roma, Lazio, 990 hivi) alikuwa mmonaki, na hatimaye abati, wa Ukristo wa Mashariki[1] katika Italia ya leo[2][3][4].

Hata Kristofa na Kali, wazazi wake na Makari, mdogo wake, walijiunga na monasteri ya Wabazili halafu wakasaidiana naye kueneza umonaki huo katika sehemu mbalimbali za Italia Kusini iliyozidi kuvurugwa na wavamizi Waislamu. Hatimaye alirudi kuishi kama mkaapweke.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi[5] kama mtakatifu, sawa na familia yake yote.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 5 Februari[6].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. Lynn White Jr. "The Byzantinization of Sicily." The American Historical Review. Vol. 42, No. 1 (Oct., 1936). p. 5.
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/39620
  3. http://www.treccani.it/enciclopedia/saba-il-giovane-santo/
  4. http://www.katolsk.no/biografier/historisk/sabbasdy
  5. Great Synaxaristes: (in Greek) Ὁ Ὅσιος Σάββας ἐκ Σικελίας. 5 Φεβρουαρίου. ΜΜεγασ Συναξαριστησ.
  6. Martyrologium Romanum
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.

.