Shetri (kundinyota)

Kwa maana mengine ya jina hili angalia hapa Shetri

Nyota za kundinyota Shetri (Puppis) katika sehemu yao ya angani
Ramani ya Shetri-Puppis

Shetri (kwa Kilatini na Kiingereza Puppis) [1] ni jina la kundinyota kwenye nusutufe ya kaskazini ya dunia yetu.

Jina hariri

Puppis (Shetri) ilianzishwa kama kundinyota ya pekee katika karne ya 18 kwa hiyo haikujulikana vile kwa mabaharia Waswahili ambayo hata hivyo waliotumia nyota zake kutafuta njia baharini wakati wa usiku.[2]

Hadi karne 19 kundinyota hii ilitazamiwa kuwa sehemu ya kundinyota kubwa zaidi iliyoitwa Argo Navis, mara nyingi pekee "Navis" (yaani merikebu) iliyokuwa moja ya kundinyota 48 zilizoorodheshwa na Klaudio Ptolemaio. Waarabu waliita Safina au Markab. Lacaille alihesabu ndani yake nyota 180 zilizokuwa nyingi mno kwa kuzitaja kwa majina ya Bayer na hivyo alianza tayari kugawa Argo Navis kwa sehemu tatu za Tanga (Vela), Mkuku (Carina) na Shetri (Puppis). Hii ilithibitishwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia katika orodha ya kundinyota 88 za kisasa iliyotolewa mwaka 1930. [3]Kifupi rasmi ni 'Pup' [4].

“Puppis” inataja shetri ambao ni sehemu ya nyuma ya merikebu au meli.

Mahali pake hariri

Shetri - Puppis lipo katika ukanda wa Njia Nyeupe, katikati ya nyota angavu mbili za Shira (Sirius) na Suheli (Canopus).

Inapakana na kundinyota jirani za Mchoraji (Pictor), Mkuku (Carina), Tanga (Vela), Dira (Pyxis), Shuja (Hydra), Monukero (Monoceros), Mbwa Mkubwa (Canis Major) na Njiwa (Columba).

Nyota hariri

Shetri - Puppis ni kundinyota kubwa yenye nyota nyingi. Haina nyota zinazoitwa Alfa au Beta kwa sababu majina haya yalitolewa tayari kwa nyota za Argo Navis kwa jumla; upande wa Mkuku zilibaki nyota ambazo majina yalianza kwa ζ Dzeta .

ζ Dzeta Puppis au “Naos" ni nyota angavu zaidi. Ina mwangaza unaoonekana wa 2.21 ikuwa na umbali unaokadiriwa kuwa miakanuru 1100[5] au 970 [6] kutoka Dunia.

π Pi Puppis ni nyota maradufu ya nyota mbili ambayo ni angavu ya kufuata humo. Ina mwangaza unaoonekana wa 2.7 ikuwa na umbali unaokadiriwa kuwa miakanuru 810 kutoka kwetu. Ndani yake ina nyota mbili, moja ni jitu wa aina ya spektra K3 Ib na mwenzake ina mag 6.86. [7]


Jina la
(Bayer)
Namba ya
Flamsteed
Jina
(Ukia)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miakanuru)
Aina ya spektra
ζ Naos au Suhail Hadar 2,21m ca. 1100 O5 IAf
π Pi Puppis 2,7m ca. 800 K3 Ib
ρ 15 ρ Rho Puppis 2,83m 64 F6 IIp
τ τ Tau Puppis 2,94m 182 K1 III
ν ν Ny Puppis 3,17m ca. 400 B8 III
σ Sigma Puppis au Hadir 3,25m ca. 194 K5 III
ξ 7 Ksi Puppis au Aspidiske 3,34m ca. 1200 G6 Ia

Tanbihi hariri

  1. Uhusika milikishi (en:genitive) ya "Puppis" katika lugha ya Kilatini ni pia "Puppis" na hili ni umbo la jina linaloonekana katika majina ya nyota za kundi hili kama vile Alfa Puppis, nk.
  2. ling. Knappert 1993
  3. The Constellations, tovuti ya International Astronomical Union , iliangaliwa Oktoba 2017
  4. "The IAU list of the 88 constellations and their abbreviations" ya mwaka 1922, kwenye tovuti ya Ian Ridpath, iliangaliwa Mei 2017
  5. Puppis], tovuti ya Constellation Guide, iliangaliwa Oktoba 2017
  6. Naos (Zeta Puppis), Tovuti ya Prof. Jim Kaler
  7. π Puppis (Pi Puppis) , tovuti ya Constellation Guide

Viungo vya Nje hariri

Marejeo hariri

  • Richard Hinckley Allen: Star-Names and their Meanings; kwa G. E. Stechert New York, Leipzig, London, Paris 1899, “Argo Navis” ukurasa 63 ff (online hapa kwenye archive.org)
  • Jan Knappert, 1993: The Swahili Names of Stars, Planets and Constellations; The Indian Ocean Review September 1993 Volume 6 No. 3 September 1993, kurasa 6-7, ISSN 1031-2331