Kikomori

(Elekezwa kutoka Shikomor)

Kikomori ni lugha asilia ya wakazi wa funguvisiwa la Komori katika Bahari Hindi. Pamoja na Kifaransa na Kiarabu ni moja ya lugha rasmi ya Komori.

Inahesabiwa kati ya lahaja za Kiswahili au kama lugha ya karibu na Kiswahili. Huandikwa kwa herufi za Kiarabu lakini kuna pia mielekeo ya kusanifisha maandishi yake kwa herufi za Kilatini.

Kwa jumla athira ya Kiarabu na Kifaransa ilikuwa kubwa, hivyo kuna maneno mengi zaidi yenye asili ya Kiarabu kuliko kwenye Kiswahili sanifu.

Kila kisiwa cha Komori huwa na lahaja yake zinazoitwa:

Ngazija - Kingazija
Nzwani - Kinzwani
Mwali - Kimwali
Mayote - Kimaore

Viungo vya Nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kikomori kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.