Shirika la Mpango wa Chakula Duniani

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (kwa Kiingereza: World Food Programme) ni tawi la kutoa msaada wa chakula la Umoja wa Mataifa na shirika kubwa zaidi la kibinadamu ulimwenguni kushughulikia njaa na kukuza usalama wa chakula.[1]

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa

Kulingana na WFP, inatoa msaada wa chakula kwa wastani wa watu milioni 91.4 katika nchi 83 kila mwaka. Kutoka makao makuu yake huko Roma na kutoka ofisi zaidi ya 80 za nchi kote ulimwenguni, WFP inafanya kazi kuwasaidia watu ambao hawawezi kuzalisha au kupata chakula cha kutosha kwa ajili yao wenyewe na ya familia zao. Ni mwanachama wa Kikundi cha Maendeleo ya Umoja wa Mataifa na kamati kuu yake.[2]

Marejeo hariri

  1. WFP. Mission Statement. WFP. Iliwekwa mnamo 2 November 2013.
  2. Executive Committee Archived 11 Mei 2011 at the Wayback Machine.. Undg.org. Retrieved on 2012-01-15

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: